Na Fadhili Athumani, Moshi
WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Tanzania, Mizengo Peter
Pinda amezindua mradi wa kuimarisha Halmashauri za miji 18 ya Dola milioni 225
inayofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya dunia.
|
Waziri mkuu Mizengo
Pinda, akipokea mkataba wa mradi wa uhimarishaji wa Halmashauri za miji 18
uliozinduliwa leo, katika manispaa ya moshi, mkoani kilimanjaro, kuotka kwa
mkurugenzi wa Benki ya Dunia, Philippe Donger, kulia ni waziri wa nchi
Tamisemi, Hawa Ghasia.picha na Fadhili Athumani.
|
Katika hafla hiyo iliyofanyika leo, katika ukumbi wa Kuringe, Manispaa ya
Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Waziri Pinda amezitaka Halmashauri zote kuhakikisha
zinajenga tabia ya kutenga Bajeti kwa ajili ya kutunza miradi yote
inayoanzishwa hapa nchini ikiwemo Barabara na mradi huo.
Waziri Mkuu Pinda ameyasema hayo katika
Warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri zote za miji 18 Tanzania
Bara iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kuringe, manispaa ya Moshi, Mkoani
Kilimanjaro, mradi uliofadhiliwa kutokana na Fedha za mkopo wa Dola milioni 225
kutoka benki ya dunia.
Pinda amesema endapo mradi huo
unaolenga kuimarisha Halmashauri ya miji 18 Tanzania bara ya Iringa, Moshi,
Tabora, Lindi, Babati, Kibaha, Geita, Mpanda, Bariadi, Sumbawanga, Shinyanga,
Songea, Morogoro, Singida, Njombe, Musoma, Korogwe na Bukoba itasimamiwa vizuri
na kutekelezwa kwa wakati itawezesha halmashauri kuibua vyanzo vingine vya
mapato.
“Mheshimiwa Rais aliagiza na mimi
narudia, Halmashauri zijenge tabia ya kutenga bajeti kwa ajili ya kutumnza
miradi inayoanzishwa ikiwemo barabara na mradi huu tunaouzindua leo,” alisema
Pinda.
Pinda amesema uzinduzi wa mradi huo ni
thibitisho wa utayari wa Tanzania kutekeleza kazi kubwa na yenye kuleta
matumaini ya maisha bora kwa wananchi wote na faraja kwa wageni watakaotembelea
miji ya Tanzania siku zijazo.
|
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda (katikati), Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Philippe
Donger kushoto) na waziri wa nchi Tamisemi, Hawa Ghasia(kulia) na baadhi ya
washiriki katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji
18 uliofadhiliwa na benki ya dunia katika picha ya pamoja jana, manispaa ya
moshi mkoani kilimanjaro.
|
Pinda ameishukuru Benki kuu ya dunia
kwa kuiteua Tanzania kwa ajili ya mradi huo ambao utekelezaji barani aferika
unaanzia nchini hapa kama mradi wa mfano huku akiwaagiza viongozi wote wa
Halmashauri zote kumi na nane, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha
mradi huo unafanikiwa .
“Wote tumesikia kuwa Tanzania ni nchi
ya kwanza katika Bara la Afrika kuteuliwa kufanya majaribio ya mfumo huu wa
kupima matokeo ya mradi. Uteuzi huu umekuja wakati muafaka ambapo nchi yetu
inaonesha imani kubwa ya jinsi serikali ilivyoamua kuwaletea maendeleo wananchi
wake,” alisema
Waziri Pinda amesema kuwa katika
utekelezaji wa mradi huo, serikali haitafumbia macho uzembe au uharibifu wa
fedha na vifaa utakaosababisha kazi hiyo kukwama na utekelezaji wa chini ya
kiwango.
“Mafaniko ya mradi huu yataongeza imani
kwa wananchi wetu, kuvutia wadau wengine kushirikiana na Halmashauri zetu
kutekeleza miradi ya maendeleo, hatufumbia macho uzembe au uharibifu wa fedha
au vifaa utakaosababisha uteklezaji wa mradi huu kukwama,” alisema Pinda.
Awali akisoma taarifa ya wizara, Kaimu
Katibu mkuu, ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI), jumanne Sagini alisema Mradi huo
uliofadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Benki ya dunia, unalenga kuimarisha uwezo wa
halmashauri za miji 18 katika utoaji huduma (Urban Local Government strengthening
programme-ULGSP).
Amesema katika kutekeleza mradi
huo, miji yote itakuwa imenufaika pakubwa na hivyo kubadilisha sura ya miji
yetu na kuifanya ivutie uwekezaji, kuishi na kufanya kazi.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya
waziri mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema mradi huo unalenga kuendelea
kuziimarisha halmashauri za miji katika maeneo makuu matano ambayo ni
Uboreshaji wa mfumo wa Mipangomiji, Ukusanyaji wa mapato ya ndani hususan
mapato yatokanayo na kodi ya majengo.
Maeneo mengine yatakayolengwa na mradi
huo ni uboreshaji wa mifumo ya udhibiti wa fedha, manunuzi ya mswala ya
mazingira na kijamii, uboreshaji wa mifumo ya utekelezaji, uendeshaji na
utunzaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma za jamii na kuboresha uwajibikaji
na uwazi.
Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha
miaka mitano, kuanzia mwaka 2013 hadi 2018 kwa mkataba kati ya Benki ya Dunia
na Serikali ya Tanzania, uliosainiwa mwezi desemba mwaka 2012 ambapo jumla ya
Dola za kimarekani milioni 225 zimetengwa huku dola milioni 201 zitapelekwa
moja kwa moja kwenye halmashauri.
|
No comments:
Post a Comment