Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MECHI ya mchujo ya Kombe
la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory
Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh.
502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Tiketi za kushuhudia
mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh.
20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo
ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh.
76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia 15 ya uwanja
sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na
asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.
Asilimia 60 ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni
asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars
dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.
Aidha, kocha wa Taifa Stars,
Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa
mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani
(CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka
huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi
ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kim amesema wachezaji
watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.
Wachezaji hao ni Juma
Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari
Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank
Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva,
John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na
Zahoro Pazi.
Mechi hiyo namba 37
dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na
14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika
Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.
No comments:
Post a Comment