Na Johnson Jabir, Moshi-Kilimanjaro
Katika kuhakikisha riadha
nchini Tanzania inafuta uteja kwa wakimbiaji wake kwa wafukuza upepo wa Kenya,
Klabu ya Holili (HYAC) ya Mkoani Kilimanjaro imedhihirisha hilo katika Taveta
Athletics Championship kwa kuwabwaga Wakenya katika mbio za meta 5000, 1500,
800 na 100.
Michuano hiyo ya Taveta
imefanyika mwishoni mwa wiki katika Kaunti ya Taita-Taveta katika Mkoa wa Pwani
nchini Kenya katika wilaya ya Taveta kwa kuwakutanisha wanariadha wa nchini
Kenya huku Holili Youth Athletics Club ikialikwa kutoka nchini Tanzania.
Katika Mbio za meta 5,000
alikuwa ni Baraka Williams aliyekimbia kwa dakika 14:45:22 nafasi ya pili
ikishikwa na Mtanzania mwingine Abubakar
Joel aliyekimbia kwa muda wa 16:00:00
na nafasi ya tatu ikashikwa na Mkenya Kivoko Makao ambaye alikimbia kwa
muda wa 16:34:00.
Wambura Lameck, Mtanzania
kutoka katika klabu ya Riadha kwa vijana (HYAC) alionyesha uwezo katika mbio za
meta 100 na 800 kwa wanaume; katika mbio za meta 100 Wambura alikimbia kwa muda
wa sekunde 12:67 akiwatupa Wakenya Walter Kamujalo (13:12), Emmanuel Paulo
(13:70) na Joseph Daudi (14:20).
Mbio za mita 800 Wambura Lameck
alikimbia kwa muda wa dakika 2:02:16 akimwacha Mkenya Ropya Nyingi ambaye
alichukua muda wa dakika 2:04::14 na nafasi ya Tatu ikishikwa na Mtanzania
kutoka HYAC Paulo Jackson aliyekimbia kwa muda wa dakika 2:05:98, Wakenya
wengine Joseph Daudi (3:00:00) na Philip Matheka (3:04) walisshika nafasi mbili
za mwisho.
Pia Watanzania waliwaonyesha
kazi nyingine Wakenya katika mbio za meta 1500 pale Baraka Williams kutoka HYAC
alipowakimbiza na kuongoza baada ya kumaliza kwa muda wa dakika 3:48:77
akifuatiwa na Mkenya Vicent Daniel kutoka Taveta aliyemaliza kwa kutumia muda
wa dakika 4:16:85 nafasi ya tatu ikishikwa na Mtanzania mwingine kutoka HYAC
Paulo Jackson ambaye alikimbia kwa dakika 5:04:66 na Mkenya Tumuna Ludovick
akikimbia kwa muda wa dakika 5:09:07.
Kwa upande wa wanawake
Watanzania Furaha Sambeke na Pendo Pamba walifanya kweli katika meta 800 kwa
kushika nafasi mbili za juu.
Furaha Sambeke anayenolewa na
Klabu ya Holili Youth Athletics alikimbia kwa muda wa dakika 2:30:00 na Pendo
Pamba akimaliza kwa dakika 3:10, nafasi ya tatu ilishikwa na Mkenya Emily
Wamboi na ya nne ikishikwa na Mkenya mwingine Cecily Kimale ambao wote
walikimbia kwa kuda wa dakika 3:22:00 na 4:12:00.
Taveta Athletics Championship
imefanyika ikiwa na makusudi ya kutengeneza Timu ya Riadha ya Taifa la Kenya
ambako mchujo rasmi utafanyika Mjini Mombasa kwa watanzania alioshinda katika
mbio hizo nao watakuwemo katika kinyang’anyiro hicho kwa ajili ya kupata uzoefu
zaidi kutokana na ukweli kwamba taifa la Kenya limekuwa bora katika riadha..
No comments:
Post a Comment