Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATU wengi walijitokeza leo katika Uwanja wa Ndege wa
Mwalimu Nyerere kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea, aliyefariki nchini
Afrika Kusini, Jumanne ya wiki iliyopita.
Wadau wakijiandaa kuupokea mwili wa Ngwea Uwanja wa Ndege, huku kila mmoja akiwa haamini kinachotokea, huku Polisi nao wakiwa tayari kulinda usalama.
Jeneza la Ngwea likibebwa tayari kupakiwa kwenye gari la kuelekea Hospitali ya Taifa, Muhimbili
Kila mmoja akilia kivyake
Huyu naye alibambwa uwanjani hapo akidaiwa kutaka kumkwapulia msanii TID katika pilika pilika za mapokezi ya mwili wa msanii Albert Mangwea.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Ngwea likijiandaa kuelekea Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Mwili huo unaagwa kesho Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Ndugu wa marehemu Albert Mangwea, wakiwa na uso wa huzuni wakipokea mwili wa Ngwea.
Mwili huo leo umehifadhiwa tena katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, wakati kesho kuanzia saa mbili asubuhi utaagwa katika Viwanja vya
Leaders Club, wakati saa sita mchana mwili huo utapelekwa mkoani Morogoro kwa
ajili ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika siku ya Alhamisi.
Umati wa watu ulifurika katika Uwanja wa Ndege, huku majonzi
na vilio vikishika hatamu kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza
kuupokea mwili huo. Wasanii wengi wa muziki walifika uwanjani, akiwapo Mrisho
Mpoto, Madee, Fid Q, Keisha, Profesa Jay na wengineo.
No comments:
Post a Comment