Na Rahimu
Kambi, Dar es Salaam
HALI ya
usiri umeendelea kutawala juu ya kifo cha msanii Albert Mangwea na kuanza
kuzusha maswali kedekede kutoka kwa wadau wa muziki hapa nchini.
Pamoja na usiri huo
kutawala, Kamati ya Mazishi na Shirikisho la Muziki Tanzania, limendelea
kuwataka Watanzania kuwa na subira juu ya msiba wa msanii huyo, ambaye sasa
mwili wake utafika kesho jioni.
Msemaji wa Kamati ya Mazishi, Adam Juma kushoto, akizungumza jambo akiwa na Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba kulia.
Rais wa Shirikisho
hilo, Addo Novemba, aliwahakikishia Watanzania kuwa mwili huo utafika kesho na kuwapa
fursa wapenzi wake kuaga siku ya Jumatano, ambapo pia utaelekea mkoani Morogoro
kwa ajili ya mazishi yake Alhamis, makaburi yaliyopo Kihonda.
Ngwea alifariki
Jumanne ya wiki iliyopita nchini Afrika Kusini, alipokuwa kwenye shughuli zake
za kimuziki, ambapo hadi sasa mwili wake upo katika Hospitali ya Dk Hellen
alipofia.
Msiba wa Ngwea kwa
sasa upo nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach, Kenneth Mangwea, ambaye pia ndio
mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi yatakayofanyika Alhamis.
Ngwea atakumbukwa na
wengi kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu
kama Bongo Fleva, akitamba na nyimbo nyingi, ukiwamo wa Gheto Langu uliotesa
katika vituo vya redio na kulitambulisha jina lake kwa wadau wa muziki.
No comments:
Post a Comment