https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, June 16, 2013

Baada ya mlipuko wa bomu Arusha jana, Uchaguzi wa kata nne wote wafutwa



Na Mwandishi Wetu, Arusha
KUTOKANA na mlipuko wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu, uchaguzi wa Kata nne jijini Arusha uliopangwa kufanyika leo umeahirishwa na kupangwa tena kufanyika Juni 30 mwaka huu.

Mlipuko uliotokea jana jijini Arusha, ndivyo ilivyoleta hali hiyo ya kumwaga damu.
Uchaguzi huo umeahirishwa huku mlipuko wa jana ambao ulitokea wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maeendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anafunga mkutano wake, ulisababisha kuzuka kwa taharuki kubwa katika mkutano huo wa kampeni.


Watu kadhaa wamehofiwa kufa katika mlipuko huo, ambao umezidi kuomnyesha kuwa hali ya amani kataika Taifa hili la Tanzania inazidi kutoweka.

Mwandishi wetu jijini Arusha, aliiambia Handeni Kwetu kuwa uchaguzi huo umeahirishwa. Bado tunafuatilia kwa kina mtifuano huo sambamba na hali za majeruhi na waliopoteza maisha.

Mlipuko huo ulitokea na kuleta wasiwasi mkubwa katika kazi za kijamii, kama vile mikutano na makongamano pale yanapohusisha watu wengi na kuleta hofu kubwa.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...