Na Mwandishi Wetu,
Dodoma
SERIKALI kwa kupitia
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira,
imetangaza kuwa uwapo wa shule za Sekondari za Kata, zinapunguza uingiaji wa
mimba kwa watoto wa kike.
Stephen Wasira, akiwa Bungeni Dodoma, picha na Maktaba yetu.
Akizungumza Bungeni
mjini Dodoma, Wasira alisema kwa sababu hiyo ipo haja ya jamii kuzitumia zaidi
kwa kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanasoma kwa ajili ya maisha yao.
Alisema mtoto wa kike
akiishia darasa la saba, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa, huku utaratibu
huo ukichangia ongezeko la watu duniani, hasa nchini Tanzania.
“Wengine wanazisema
shule za kata, lakini zimechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya watoto wetu
wasome na kuacha kupata mimba wakiwa katika umri mdogo.
“Mara nyingi binti
akikomea darasa la saba tu, kupata mimba kwake ni rahisi, hivyo jamii iendelee
kuwasimamia zaidi watoto wetu ili wasome zaidi kwa ajili ya maisha yao, huku
katika suala la uongezeko la watu likipungua kwa kiasi Fulani,” alisema
Wasira.
Bunge la Bajeti
linaendelea mjini Dodoma, huku wiki hii kuanzia leo Jumatatu, Bajeti hiyo ya
mwaka 2013/2014 ikitarajiwa kupitishwa kama ratiba inavyojulikana.
No comments:
Post a Comment