Na Mwandishi Wetu, Arusha
WATU watatu wamedaiwa kufa leo
jijini Arusha, baada ya kutokea machafuko yaliyosababisha upigwaji wa mabomu na
wananchi kuzagaa ovyo mitaani. Aidha zipo taarifa kuwa Mbunge Tundu Lissu
amevunjika mguu katika pilika pilika hizo.
Hali ilivyokuwa jijini Arusha leo.
Mwandishi wetu jijini Arusha
alitupasha kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilikuwa kikifanya
mkutano bila kupewa kibali maalum kutoka polisi, ikiwa ni siku moja baada ya
kuzuiwa kukusanyika bila utaratibu.
Wabunge wanne wa Chadema,
wamekamatwa na polisi kutokana na kufanya mkutano wao katika Uwanja wa Soweto bila
kupata kibali kutoka jeshi la Polisi.
Kamishina wa Polisi Paulo Chagonja,
alisema viongozi wa Chadema waliokamatwa ni pamoja na Tundu Lissu, Mustafa Akoonay,
Said Arf na Joyce Nkya, huku Freeman Mbowe akifanikiwa kutimua mbio.
Kwa siku kadhaa sasa jiji la
Arusha limekuwa kwenye mshike mshike wa aina yake, huku hatua za awali zikisema
kuwa bomu lililorushwa katika Mkutano wa Chadema limetengenezwa nchini China.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
alitembelea majeruhi na wafiwa katika
jiji la Arusha, huku akisema kuwa serikali itagharamia kwa kiasi kikubwa juu ya
mahitaji ya walioathirika na bomu hilo pamoja na kugharamia pia mazishi ya
waliofariki.
Katika hatua nyingine, Jeshi la
Polisi limemtaka Mbowe awasilishe haraka ushahidi juu ya mtu anayehusika na
ulipuaji wa bomu kama alivyotangaza mwenyewe baada ya mlipuko huo.
No comments:
Post a Comment