https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, June 28, 2014

Airtel yazindua simu mpya ya iphone 5s

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo (kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo ( kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo ( wa pili kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
·Ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano nchini kuingia mkataba wa ushirikiano na Apple
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma bora na nafuu leo imetangaza ushirika wake na kampuni kubwa inayotengeneza simu za mkononi ya Apple.
Airtel imeweka historia kwa kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiiliano nchini Tanzania kuingia mkataba na Apple kupitia simu ya iPhone S5.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu huo jijini Dar es Saalam Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo alisema” leo tunazindua  simu ya iPhone 5s na kuwapatia wateja wetu ofa kabambe ya vifurushi vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet. Mteja atakaponunua simu ya iphone S5 atapata kifurushi cha internet cha 3GB, dakika 1450 za maongezi na SMS 5000 kwa mwezi. Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kutumbelea maduka yetu na mawakala wetu ili kuweza kujipatia simu hii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi, Beatrice Singano alisema “Uzinduzi huu leo utato fulsa kwa wateja wetu  kupata uzoefu tofauti wa huduma zetu na kuwawezesha  kuendelea kufurahia huduma yetu ya SWITCH on, huduma ambayo imezinduliwa ili kuwawezesha wateja wetu kupata internet yenye kasi zaidi bila kikomo kupitia mtandao wa Airtel”
“Simu hii ya iPhone 5s itawawezesha wateja wetu pia kupiga picha, kutuma video na kuwaunganisha na marafiki na familia .
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu ofa hii ya simu ya iPhone 5s tembelea tovuti yawww.apple.com/phone “aliongeza mmbando.

Waajiri Tanzania wapigwa mkwara mzito

 Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakifatilia mada mjini Dodoma leo.


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imepanga  kuwachukulia hatua waajiri wote nchini kwa kushindwa kuwasilisha taarifa  za wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na Bodi hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona alipokuwa akitoa mada kuhusu
urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa
Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.

“Mpaka sasa tumewachukulia hatua jumla ya waajiri watano ambao wameshindwa kuwasilisha taarifa za watumishi wao  wanaodaiwa na
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu” alisema Bw.Robert.


Alisema, mwajiri atakayeshindwa kutoa taarifa za wahitimu wa elimu ya juu katika Bodi kwa wakati atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kutumikia kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja. Aidha,Bw. Robert alisema kuwa mpaka sasa takribani waajiriwa 18 wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

Timu ya Kurugenzi ya Mufindi yajipanga


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaaam

TIMU ya soka ya Kurugenzi Mufindi iliyopo Ligi Daraja la Kwanza, imejipanga vilivyo kuhakikisha inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2015/16.

Meneja wa timu hiyo, Athuman Kihamia ambaye ni Mweka Hazina wa Halmashauri wa Wilaya ya Mufundi, ameliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kuwa wameunda uongozi mpya ili kufanikisha azma ya hiyo.

Alisema kuwa viongozi hao ni watumishi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya Mufindi, wamiliki wa timu hiyo ambayo msimu uliopita ilipambana vilivyo, lakini ilishindwa kupanda daraja kutokana na sababu mbalimbali.

“Viongozi wote wametoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufundi kwa sababu ndiyo inayoigharamia timu kwa kila kitu, lakini tutaunganana viongozi wengine wawili, Mweka Hazina na Katibu Msaidizi watakaopendekezwa na Chama cha Soka Wilaya ya Mufundi,” 
alisema Kihamia ambaye ni mmoja wa wadau maarufu wa soka jijini Dar es Salaam, kwa sasa akiwa ni mtumishi wa halmashauri hiyo.

Kihamia alisema uamuzi huo wa kuunda uongozi mpya, ulifikiwa katika kikao chao cha Juni 17, mwaka huu ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Paul Ntinika, amepania kuifikisha mbali timu hiyo, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi-kuendeleza michezo kwa vijana kama sehemu ya kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini.

Aliwataja viongozi wapya wa timu hiyo na nafasi zao kwenye mabano kuwa ni Ofisa Utumishi na Utawala Monica Andrew (Mwenyekiti), Mhandisi Ujenzi Peter Mawere (Makamu Mwenyekiti), Ofisa Mipango Miji Bernard Kajembe (Katibu Mkuu) na Mweka Hazina Athuman Kihamia (Meneja).

“Mwenyekiti Monica amechaguliwa kutokana na uzoefu wake katika soka kwani ni mmoja wa waasisi wa timu ya Mbeya City inayotesa Ligi Kuu kwa sasa,” alisema Kihamia na kusisitiza kuwa watafanya usajili wa nguvu kufanikisha azma yao ya kuifanya Mufindi kuwa na timu Ligi Kuu.

Evans Aveva amaliza kampeni kwa mbwembwe za aina yake


 Mgombea wa nafasi ya urais Evans Aveva, akiwa na Mlinzi wake 'Board Guard' (nyuma) akijinadi kwa wanachama, wakati wa mkutano wake wa kampeni za mwisho na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo kesho, kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuiongoza Klabu ya Simba kwa kipindi kijacho cha miaka minne. Hitimisho hilo la kampeni zake limefanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, akimnadi mgombea Urais Evans Aveva.
 Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.

Friday, June 27, 2014

TANGAZO: HANDENI KWETU FOUNDATION

Taasisi ya Handeni Kwetu inapenda kukutangazia kuwa fomu tayari zimefika wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kuanzia leo Juni 27, yoyote anayependa kuchukua fomu hizo anashauriwa kufika ofisini, mtaa wa Mdoe, nyumba namba 10061, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Aidha unashauriwa pia kuchukua fomu sambamba na Katiba kwa ajili ya kuipitia kabla ya kuamua kujiunga kuwa mwanachama. Taasisi inapenda kuwasisitiza Watanzania wote kujitokeza katika zoezi la uchukuaji fomu ili wafanikishe mustakabali wa taasisi na maendeleo ya Handeni na Taifa kwa ujumla.

Fika ofisini au piaga simu +255 684460116 au +255 762 971062. Namba binafsi za viongozi ni kwa Handeni ni mwenyekiti +255 653433245 na Katibu wake ni +255 718372741.
Kwa Dar es Salaam unaweza kuipata fomu hii kupitia kwa Sanura Ally, namba yake ni 0713 766017, Yasin Mohamed 0713420242 au kwa Kambi Mbwana......

Imetolewa na Kambi Mbwana, Msemaji Mkuu
P.o Box 79, Handeni,
Email ya taasisi: handeni.foundation@gmail.com
Email Binafsi: kambimbwana@gmail.com
Simu Binafsi: +255 712053949

Thursday, June 26, 2014

Yanga waula, Marcio Maximo atua Dar na kulakiwa na amshabiki wa Yanga


Marcio Maximo wakati anawasili Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kuingia mkataba na klabu ya Yanga.
KOCHA wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Marcimo Maximo, amewasili nchini leo kwa ajili ya kuwa kocha mpya wa Yanga.

Maximo alitua katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere saa nane mchana kwa Shirika la Ndege ya Afrika Kusini, akiwa  na kocha msaidizi wake, Leonaado Neiva na kulakiwa na mashabiki wa Yanga waliojitokeza kumpokea.

Mara baada ya kuwasili Maximo  alipokelewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu na Ofisa habari wa klabu hiyo,  Baraka Kizuguto.

Kocha huyo ilimchukua muda wa nusu saa kutoka nje kufuatia kukamilisha taratibu ya Uhamiaji na kuvalisha stafu ya Yanga.

Tuesday, June 24, 2014

Ilala yasaini mkataba mnono wa maji

 Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa Akiwasili kata ya Kipunguni na kupokelewa na Diwani wa kata Hiyo Na Viongozi wengine .
 Mkandarasi wa kampuni Kika Construction Mbaraka Kihawe akimkaribisha Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kwenye meza kuu.
 Mwanainchi Huyu alipatwa na Furaha sana Kumuona Mh Jery Silaa akashindwa kujizuia na kwenda Kumsalia.

Monday, June 23, 2014

Mb Dog akamilisha mbili mpya bomba balaa


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amekamilisha nyimbo nyingine mbili mpya zinazojulikana kama Ya Moto na Demu Mwingine.


Msanii Mb Dog pichani.
Kukamilika kwa nyimbo hizo ni mwendelezo wa mikakati ya msanii huyo kufanya kazi nzuri ili kumuweka katika kiwango cha juu katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Akizungumza leo mchanaa jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema kwamba nyimbo hizo amezirekodi katika Studio yake ya Macoppa, zilizopo jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa nyimbo hizo zinaungana na ile ‘Mbona Umenuna’ aliyoachia mapema mwezi uliopita na kupokewa kwa shangwe na wadau wa Bongo Fleva Tanzania.

“Hizi ni nyimbo mbili mpya na ambazo naamini zitapokewa kwa shangwe na wadau mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.

“Naamini kila kitu kitakwenda vizuri kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa mazuri, ukizingatia kuwa mipango iliyopo mbele yangu ni kufanya kazi ya maana ili nionyeshe ukomavu wangu kisanaa,” alisema Mb Dog.

Mb Dog ni mmoja wa wasanii wanaotambulika kwa umahiri wao katika tasnia ya Bongo Fleva, huku akikumbukwa kwa nyimbo zake, ukiwamo ule wa Latifa na nyinginezo.

Taifa Stars kuelekea kesho Botswana kuweka kambi ya wiki mbili

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

TIMU ya Taifa (Taifa Stars), inaondoka kesho alfajiri kuelekea nchini Botswana kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Msumbiji.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kwamba maandalizi kwa ajili ya safari ya Stars yamekamilika.

Alisema timu hiyo itaweka kambi Botswana kwa wiki mbili kabla ya kurudi Tanzania, ambapo watakuwa wamejiweka sawa kuvaana na Msumbiji.

“Kila kitu kipo sawa kwa ajili ya safari ya Stars ambayo vijana wataweka kambi ya wiki mbili, huku tukiamini kuwa yatakuwa mazoezi mazuri.

“TFF na Watanzania wote tunadhani huu ni wakati muafaka kwetu kuiwekea mazingira mazuri Taifa Stars ili iweze kuonyesha soka zuri,” alisema.

Kwa mujibu wa Wambura, Taifa Stars itaondoka kesho alfajiri na Shirika la Ndege la Afrika Kusini kwa ajili ya kuelekea nchini Botswana kuweka kambi ya wiki mbili.

TFF yajisalimisha bungeni Dodoma

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukiongozwa na Jamal Malinzi juzi mjini Dodoma umekutana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mtanda (Mbunge wa Mchunga).


Katika kikao hicho TFF ilielezea mikakati yake ya maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Msumbiji.


TFF iliiahidi Kamati ya Bunge kuwa itaendelea kuwa inafanya shughuli zake kwa karibu na Serikali na kamati hiyo ya Bunge.

Katika kikao hicho, ujumbe wa benki ya CRDB ukiongozwa na Meneja wa Electronic Banking, Bw. Mangire Kibanda ulihudhuria ili kutoa ufafanuzi juu ya mradi wa kuuza tiketi za elektroniki, mradi ambao maandalizi yanaendelea vizuri.

Sunday, June 22, 2014

Yanga yawakalia kooni wanafiki



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, imewataka wanachama wenye mapenzi mema na klabu yao kusikiliza habari kutoka ndani ya uongozi na sio zinazotoka kwa wanaopenda kuzalisha migogoro klabuni kwao.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kulia akiwa na Msemaji wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto katika matukio ya klabu hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kwamba mengi yanayoibuliwa na watu hao yanatokana na kuwa na malengo ya kuivuruga klabu yao.

Alisema kwamba baadhi ya watu hao wamekuwa wakiibua hoja nyepesi, ikiwamo ya mkutano wa dharula kwa ajili ya kuleta matatizo klabuni kwao, hivyo kila anayeipenda klabu hiyo anapaswa kusikiliza habari kutoka ndani ya uongozi wao na si zile zinatolewa kienyeji.

“Yote yanayofanywa ni kwa ajili ya klabu ya Yanga, hivyo nadhani kila mwenye mapenzi mema na timu hii anapaswa kuwa makini na kusikiliza maneno kutoka kwenye uongozi, ikiwamo hatua ya kujiorodhesha kwa wale wasioafiki uamuzi wa Juni Mosi mwaka huu.

“Watu hao hawana mapenzi mema na Yanga, ndio maana wanaweza pia kugomea hatua ya kuorodhesha majina, ukizingatia wanachotaka wao ni kuona klabu yetu inashindwa kuweka mipango ya kimaendeleo,” alisema.

Hatua ya kuanza kuorodhesha majina ya wanachama wasioridhishwa na kuongeza muda wa Uchaguzi Mkuu, imetangazwa juzi na mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, huku ikianza leo na kufikia tamati Jumamosi.

Sunday, June 15, 2014

Uchaguzi Mkuu Simba wasimamishwa hadi kuundwa kwa Kamati ya Maadili Simba



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), limeusimamisha Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Simba, hadi hapo watakapofanikiwa kuunda kwa Kamati ya Maadili itakayokuwa na jukumu la kusikiliza malalamiko yote yanayohusiana na wagombea wao.

Kusimamishwa huko kumekuja siku chache baada ya mchakato wa uchaguzi wa Simba kuanza, ambapo Kamati ya Uchaguzi ya Simba, chini ya Damas Ndumbaro ilimuengua Michael Wambura kuwania Urais wa klabu hiyo, kabla ya Kamati ya Rufaa kumrudisha kwa madai kuwa uovu upo kwa Simba, si Wambura.

Akizungumzia hilo leo mchana, jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, alisema kuwa Simba inapaswa kuunda Kamati ya Maadili kabla ya Juni 30 ili kusikiliza mashauri yatakayoletwa mbele yake na kuyatolea ufafanuzi, jambo ambalo huenda likapokewa kwa shingo upande wa wadau wa soka Tanzania, maana klabu hiyo imetumia gharama hususan wale waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

 

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...