KOCHA Mkuu wa timu ya
Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, amesema kwa sasa wameacha kwanza suala la usajili
hadi watakapogundua kuwa timu kongwe za Simba na Yanga zimemaliza, ili kuepusha
migogoro inayotokea mara kwa mara kutokana na kuchukua hata wale walioingia
mkataba na timu nyingine.
Mexky Mexime, Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar
Sakata la usajili kwa
klabu za Ligi Kuu limeibua msisimko wa aina yake, huku timu za Simba, Yanga na
Coastal Union zikionekana kugongana vichwa kwa ajili ya kuboresha vikosi vyao.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mexime alisema kuwa mara nyingi timu za Simba na Yanga
zimekuwa zikileta vurugu katika suala zima la usajili, hivyo wameamua kwanza
wasubiri wao wamalize ndio wasajili, hasa kwa kuangalia mnyukano unaoendelea.
Alisema wao wanaamini
kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka, hivyo hawawezi
kuathiriwa, hasa kwa kuamua kupisha keleleza Simba na Yanga.
“Unaweza kumsajili
mchezaji au kuwa na mipango naye, lakini inapotokea anawindwa na Simba au
Yanga, basi huwa kwenye matatizo ya kila aina, hivyo ni bora wafanye kwanza
wao.
“Sisi tupo imara na
tunajiamini, ndio maana tuna uwezo wa kuchukua hata wale ambao wanaona si
lolote na kuwapika ndani ya timu yetu, wakati wao wanasubiri wale
waliotengenezwa,” alisema.
Kwa mujibu wa Mexime,
uamuzi huo uliangaliwa kwa kina na kusema kamwe hauwezi kuwaathiri kwa
kutangaza kuacha kusajili hadi Simba na Yanga wamalize, ikiwa ni njia ya
kuepusha mkanganyiko kwenye mpira wa miguu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment