Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MASHINDANO ya Riadha
ya Tabora Marathon yaliyopangwa kufanyika leo mjini Tabora, yameahirishwa.
Mshauri wa Ufundi wa Tabora Marathon, Tullo Chambo kushoto akizungumza jambo juu ya mashindano hayo.
Akizungumza jana kwa
njia ya simu kutoka Tabora, Mshauri wa Ufundi wa Tabora Marathon, Tullo Chambo,
alisema kuahirishwa kwa mashindano hayo kumetokana na sababu zilizokuwa nje ya
uwezo wao.
Alisema baada ya
kuahirishwa huko, sasa mbio hizo zitafanyika wiki ijayo endapo mambo yataka
sawa.
Chambo alisema japo
kila kitu kilikuwa kimekamilika, lakini kati ya vitu vilivyotarajiwa kuwapo katika
mashindano hayo, kilichelewa kupatikana, hivyo kulazimika kuahirisha kwa ajili
ya kuhakikisha kuwa mbio hizo zinakuwa na mafanikio makubwa.
“Sisi kama wadau wa
riadha tuna mipango ya kuona mashinxdano haya yanakuwa na mvuto mkubwa mkoani
Tabora.
“Katika hili naamini
hata kuahirisha huko kutakuwa ni sehemu ya kuiweka riadha katika kilele cha
mafanikio,” alisema.
Tayari wadau wa
mashindano hayo wameshawasili mkoani Tabora kwa ajili ya kuhakikisha kuwa
Tabora Marathon yanafanyika kwa mafanikio makubwa mjini humo.
No comments:
Post a Comment