https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, February 10, 2013

Umeshawahi kumdekeza mpenzi wako?



MAMBO FULANI MUHIMU
Picha inajieleza kabisa. Hawa ni wapenzi wanaofurahia 'love yao'.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIKA suala zima la mapenzi, kuna baadhi ya vitu ambavyo ukikutana navyo unaweza kushikwa na bumbuwazi. Ni pale mtu anapotumia muda mwingi kushindana na mtu wake.

Ni ngumu sana. Ni wakati wa kila mtu kujua kuwa, binadamu tupo kwa jinia mbili tofauti. Alivyoumbwa mwanamume si sawa na alivyoumbwa mwanamke.

Katika hilo, viumbe hivi viwili, kila moja ina hulka yake. Kwa mwanamke, mara kadhaa amezoea kudekezwa hasa katika suala zima la mapenzi, anapogundua yupo kwa mtu anayempenda.

Mwanamke wa aina yoyote, hata kama awe na umbo gani, lakini bado atakuwa chini, akijitia madeko kila anavyopenda. Si vibaya, hasa kama anamdekea mpenzi au mume wake.


Kutokana na hilo, sisi wanaume ni lazima tujuwe namna ya kuishi na viumbe hawa ili kuwapatia raha zaidi. Si vizuri kuwa wakali muda wote hadi kufikia kuwaogopesha.

Tukifanya hivyo, hamu ya kuwa na waume zao kila mara inakwisha, hasa kwasababu ya kero, matatizo ya kushindwa kujua unavyokaa na mwanaume mwenzako tofauti na mwanamke.

Hata kama uwe na pumzi vipi katika suala zima la mapenzi, lakini kwasababu huwezi kuwa mbunifu, kujua kudekeza, mpenzi wako, mke wako hawezi kujisikia raha kuwa na wewe kila wakati.

Zaidi, atakuwa radhi kutumia muda wake mwingi kuzungumza na marafiki zake, ndugu zake, akisingizia kila anavyoona inafaa, maana wewe sio mtu wa kumpa raha zaidi ya karaha.

Ingawa madeko yakizidi pia si mazuri, lakini pia lazima mtu ajuwe hakuna mwanamke ambaye hapendi kudekezwa. Na anapogundua wewe tabia hiyo huna, hakika atakuwa mnyonge.

Haya si mapenzi ya kuiga. Maana hata kwa wanaume, baadhi yao nao huona raha kudeka kwa wasichana wao. Haya ndio mapenzi, hasa yanapotokea watu wote wanapenda kwa dhati.

Endapo mmoja wapo hana upendo wa dhati kwako, hakika hawezi kukubali umdekee, au akudekee bila sababu za msingi. Huo ndio ukweli, hivyo ifikie wakati tujuwe namna ya kuishi na watu wetu.

Samahani, kusema mpenzi, sina maana kuwa sizungumzii ndoa zaidi ya wapenzi tu kama alivyowahi kusema msomaji wangu mmoja, aliyetaka nizame zaidi kwa watu waliofunga ndoa.

Ni maoni yake, lakini wengi wanaopitia katika uchumba, upenzi, baadhi yao ndio wanaokuwa wana ndoa. Tuombe Mungu, ila pamoja na hayo yote, hata wenye ndoa zao, wakati mwingine kudekeana ipo.

Mtu anaweza kujifanya ni mgonjwa sana. Kumbe mwongo tu. Ukimwambia basi ingia chumbani ukalale, hataki, anataka alale sebuleni tu.

Ila ukiendelea kumliwaza, kumshika hapa na pale, kumpa maneno matamu ya mahaba, kujikunja kwake kunakwisha na badala yake hisia za sita kwa sita zinamjia, hivyo kuingia mchezoni.

Hata kama mwanaume hakuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa, lakini kwakuwa amemkuta mpenzi, au mke wake yupo katika hali ya unyonge, naye akatumia uanaume wake, anajikuta anataka kulipa deni la kudeka kwa mtu huyo ambaye mwisho wa siku hujikuta akivuja jasho la furaha.

Lakini kwa bahati mbaya, wenzangu na mimi wanapowakuta wapenzi wao wamekaa, wakitaka kudeka, nao hukunja uso, maana hawataki kudekewa hivyo kuwanyong’onyeza zaidi.

“Usitake kunisumbua bwana. Sasa kama unaumwa, au hujielewi si uende hospitali kuliko kunidekea mimi,” hizi ni kauli za kusikitisha kama zinatokana katika kinywa cha mwanaume.

Mbaya zaidi, kesho wanaume hao huanza kulalamika kuwa wananyimwa unyumba, yani tendo la ndoa. Huu ni ujinga kabisa. Ni jambo gumu mwanamke kutamka kuwa anataka kitu fulani.

Zaidi huonyesha hisia kwa njia mbalimbali,  ikiwamo kudeka, hivyo wewe kama hutaki basi itakula kwako. Nadhani kwa kulijua hilo, tuna kila sababu ya kuangalia mwenendo wetu.

Lazima tujuwe pia mwanamke ili aweze kutulia ni lazima ajuwe kwako akideka, atabembelezwa kwa sababu mbalimbali, hivyo ukali hausaidii, hasa ukijua mwanamke huyo ni chaguo lako sahihi.

Raha ya mapenzi hapo ndipo inapokolea. Vinginevyo, tutayaona machungu na yenye ukakasi mkubwa.
Tukutane wiki ijayo.
kambimbwana@yahoo.com
0712 053949
0753 806087

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...