Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewapiga marufuku kuingia bungeni wabunge wote
ndani ya chama chao, badala yake waelekee jijini Arusha kwa ajili ya kuomboleza
vifo vya waliolipukiwa na kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Kauli ya Mbowe ni kama kususia
vikao vya Bunge la Bajeti, ambalo linaendelea mjini Dodoma, ikiwa ni siku
chache baada ya mlipuko huo kutokea jijini Arusha wakati yeye mwenyewe anafunga
mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Kata nne, ambapo sasa uchaguzi huo umepelekwa
mbele hadi Juni 30 mwaka huu.
Akizungumza juu ya mgomo huo,
Mbowe alisema wabunge wake kutoka Chadema, hawawezi kuingia bungeni badala yake
amewaelekeza waende Arusha kwa ajili ya maombolezo ya watu wanaowaunga mkono,
licha ya kulipukiwa na kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu.
Alisema kwa sasa hawawezi
kusema lolote juu ya kadhia hiyo iliyosababisa vifo vya watu wawili na wengine
kadhaa kujeruhiwa, isipokuwa kuacha kuingia bungeni ili waungane na wananchi wa
Arusha juu ya tukio hilo la aina yake.
“Nimewaelekeza wabunge wetu
wote kutoka Chadema kuwa hakuna haja ya kuingia bungeni katika Bunge la Bajeti
ili tushiriki katika maombolezo haya ya watu waliokufa baada ya mlipuko huo,”
alisema Mbowe.
Kauli ya Mbowe imepokelewa kwa
hisia mbili tofauati, wakiwapo wale wanaomuunga mkono kutoka Chadema na wale
wanaompinga yeye na chama chake kwa madai kuwa hakuna haja ya wabunge wote
kwenda Arusha na kuacha bajeti inayoweza kuwanufaisha Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment