Na Cathbert Angelo, Dar es Salaam
SHINDANO la Redd’S Miss Kinondoni Talent 2013 linatarajiwa kufanyika
alhamisi ya Juni 25 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam ambalo litashirikisha warembo wapatao kumi na mbili ambao watachuana
kumpata mrembo mwenye kipaji.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari
(hawapo pichani), kwa sasa warembo hao wameshaingia katika hoteli ya JB Belmont
jijini Dar es Salaam kujinoa kwa ajili ya Redd's Miss
Kinondoni Talent 2013 zinazofanyikia ukumbi wa Shekinah Garden Mbezi
Beach na Fainali zinafanyika Juni 21 ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip.
Akizungumza mratibu wa shindano
hilo, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea
vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano
hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden
Tulip.
“Ninachoweza kusema shindano la
mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto
na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao “Alisema Ssebo.
Warembo warembo wanaotarajiwa
kumenyana ni kutoka katika vitongoji vya Sinza, Ubungo na Dar Indian Ocean
ambao kwa pamoja wanaunda Redd's Miss Kinondoni 2013.
Alisema kwamba shindano la mwaka
huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana
wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya
urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano ya Redd's Miss
Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame
Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group,
Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim
Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher,
Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment