Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DIWANI
wa viti Maalum Ilala, Eshe Sururu ameahidi kuwasaidia wajasiriamali zaidi ya
1125, kuwatafutia fursa za mikopo nafuu, na kuwatafutia shamba hekari 100 kwa
ajili ya kilimo cha biashara.
Alitoa
ahadi hiyo juzi, wakati akikaribishwa kuwa mlezi wa vikundi 46 vya
wajasiriamali, vilivyopo chini ya Jumuia ya Kukuza Uchumi Ilala (JUKUILA).
Alifurahishwa
na mikakati ya baadhi ya vikundi hivyo kwa kuwashirikisha watoto kwenye elimu
ya ujasiriamali, na kutoa sh. 100,000 kwa ajili ya kufungua akaunti ya pamoja
ya watoto ili iwasaidie kwenye kuwekeza fedha za kuwasomesha.
Alisema,
familia nyingi katika vikundi hivyo, vina watoto waliomaliza masomo bila ya
kuwa na mkakati wowote wa kimaendeleo.
"Tutafanya
harambee kubwa ya kuhakikishahakuna mtoto anayekaa nyumbani, bali wote
wanaendelea na masomo kwa ngazi waliyoishia.
"Hatutaki
kuwa na Tanzania yenye vibaka, wavuta unga na bangi, tunaka kuijenga nchi yenye
vijana waadilifu na wachapakazi, na serikali ya CCM inatekeleza hili kwa
vitendo,"aliongeza.
Mwalimu
anayefundisha ujasiriamali kwenye vikundi hivyo, Esther Hosea, aliwahimiza
wanachama kukopa kwa ajili ya maendeleo, na kurudisha mikopo kwa wakati ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aliwahimiza kutangaza
bidhaa zao ambazo kwa asilimia kubwa wanatengeneza kwa mikono yao, kushirikiana
na kuepuka majungu ili kuviimarisha vikundi vyao.
Diwani wa viti maalum
Ilala, Eshe Sururu (kulia), akikabidhi msaada wa viti 100 kwa kikundi cha
wajasiriamali cha Wapendwa katika sherehe ya kukubali kulea vikundi 46, vyenye
wanachama 1125, iliyofanyika Dar es salaam juzi. Vikundi hivyo vipo chini ya
Jumuia ya Kukuza Uchumi Ilala (JUKUILA)
No comments:
Post a Comment