https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Friday, May 31, 2013

Kampuni ya Clouds Media Group yakiri kujitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kutoka Afrika Kusini hadi Tanzania kwa mazishi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Clouds FM, imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa ajili ya kuutoa Afrika Kusini hadi Tanzania kwa ajili ya kuzikwa, ukiwa ni utaratibu unaoonyesha kuwa wadau wote wameamua kushirikiana katika suala hili.
Barua inayoonyesha walioanza kuchangia msiba wa Ngwea
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, alithibitisha kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya nyota huyo wa Bongo Fleva.
                                 Marehemu Albert Mangwea
Taarifa za Kampuni hiyo kusaidia zilianza kuenea tangu juzi, baada ya Kamati ya Mazishi kushindwa kutaja makampuni, taasisi na watu walioanza kuchangia kwenye msiba huo.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
"Tumeamua kwa mikono miwili kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea,” alisema kwa ufupi.

Ngwea amepangwa kuletwa Tanzania kesho Jumamosi na kuagwa Jumapili, kabla ya kupelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake.

Ripoti ya kuteswa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd, Absalom KibandaAbslom Kibanda.

    UTANGULIZI:Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.Tukio hilo liliishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa ujumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lilomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madkatari Tanzania, Dk.

Ngwea kulala kwanza Muhimbili kesho akiletwa nchini, wakati P-Funk afunga mdomo juu ya kuwapiga biti Clouds FMNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HUKU wakikanusha ripoti  za awali zinazoendelea kusambaa juu ripoti ya kifo cha msanii Albert Mangwea, Kamati ya Mazishi ya msaniii huyo, imesema kuwa inatarajia kuuleta mwili wa marehemu huyo kesho kama ilivyopangwa na kuuaga Jumapili katika Viwanja vya Leaders Club, baada ya kulala katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa siku moja.
                                 Marehemu Mangwea
Mangwea moja ya wasanii nyota hapa nchini alifariki nchini Afrika Kusini na kuzua huzuni kubwa kwa wadau wa muziki na Watanzania kwa ujumla, hasa kutokana na umahiri wake kwenye kazi hiyo, huku kifo chake kikipokelewa kwa masikitiko makubwa mno na redio zote kusikika mara kwa mara nyimbo zake zikipigwa kama sehemu ya kuomboleza msiba wa msanii huyo nyota.
                               P-Funk Majani
Mara baada ya kuwasili kesho, mwili wa marehemu utafikia kwanza katika Hospitali ya Muhimbili huku siku inayofuata ratiba zilizopangwa kuendelea kwa ajili ya kuustili mwili wake.

Thursday, May 30, 2013

Pitia matokeo ya kidato cha nne, ufaulu waongezeka tofauti na ilivyotangazwa awali

MATOKEO ya kidato cha nne yametangazwa leo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, huku akisema kuwa ufaulu umeongezeka tofauti na ilivyotangazwa awali. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa
INGIA KATIKA LINK HII KUYACHEKI http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/CSEE_2012/olevel.htm

Shindano la QS Queens kufanyika Dar Live Jumamosi sambamba na kuomboleza msiba wa Albert Mangwea, Dar Live
Kutumika pia kama sehemu ya kuomboleza msiba wa Ngwea na kushirikisha wakali kibao kama vile Mb Dog, Madee, Diamond, Nay wa Mitego na wengineo

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ONYESHO kubwa ambalo ni uzinduzi wa Shindano la QS Queens linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ya kesho ya Juni Mosi katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, pia limepangwa kuwa sehemu maalum ya kuenzi mchango wa msanii Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini.
 Diam0nd kushoto na Ney wa Mitego kulia kumenyana tena katika Ukumbi wa Dar Live Jumamosi, Mb Dog, Madee, Juma Nature na wengine kibaaao.

Watanzania wapewa namba za kuchangia msiba wa Ngwea na huku ikitangazwa kuwa ripoti zilizosambaa jana juu ya kifo chake ni za uongo Namba za Mchango wa Msiba ni 0754 074323 au 0658 074324.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMATI ya Mazishi ya msanii Albert Mangwea aliyefia nchini Afrika Kusini, imewataka Watanzania wote kuungana juu ya kufanikisha kuuleta mwili wa msanii huyo na kufanikiwa kuuweka kwenye nyumba ya milele.
Hayo yamesemwa leo mchana jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Kamati hiyo, Adam Juma, ambaye pia ameshirikiana na Shirikisho la Muziki Tanzania, chini ya uongozi wake Addo Novemba.

Juma alisema kuwa gharama ni kubwa mno kuuleta mwili huo, hivyo wadau na taasisi kwa pamoja washirikiane ili kuhakikisha kuwa msanii huyo analetwa na kuzikwa mkoani Morogoro.

Rais Tenga kuzindua kozi ya Makocha JumatatuNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UKUMBI wa Hobours Club, uliopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) itakayofanyika Jumatatu (Juni 3, 2013) kwenye 
Mkurugenzi wa Ufundi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Joseph Kanakamfumu, alisema Rais Tenga atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi hiyo itakayohusisha amakocha 26.
                                    Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Alisema kozi hiyo itakayomalizika Juni 28 itakuwa imewezesha kupatikana makocha watakaosaidia maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla.

Balozi wa Tanzania Ethiopia awapa somo Taifa StarsNa Mwandishi Wetu, Ethiopia
BALOZI wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
                             Nyota wa Taifa Stars, Mrisho Ngassa
Ametoa changamoto hiyo wakati alipotembelea mazoezi ya timu hiyo jana (Mei 29 mwaka huu). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi nchini Ethiopia na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa.

Wednesday, May 29, 2013

Nafasi kibao za kazi zatangazwa Hospitali ya Taifa MuhimbiliHospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetangaza mamia ya nafasi za ajira kwa idara tofauti, wakiwamo madaktari bingwa na wauguzi wa vitengo, vikiwamo vya watoto na upasuaji wa moyo.

Pitia tamko lote juu ya Ngwea na M to the P kutoka Shirikisho la Muziki Tanzania, ujuwe kinachoendelea kuhusu kifo cha Ngwea


TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI

Shirikisho la Muziki Tanzania (Tanzania Music Federation) tunasikitika kutangaza kifo vya msanii  ALBERT MANGWEA kilichotokea Afrika ya Kusini akiwa kwenye shughuli zake za kimuziki . Tunawapa pole Wazazi, ndugu, jamaa na watanzania wote kwa kuondokewa na mwanamuziki huyo mkongwe wa kizazi kipya, marehemu tutamkumbuka kwa mengi hasa msimamo aliounesha katika mambo aliyoyaamini, Alikuwa ni mtu mwenye jitihada hata mauti ilipomkuta alikua kwenye kujitafutia riziki.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba
Marehemu alitambulika sana katika tasnia ya muziki kupitia wimbo wa GETO LANGU TU na baadae alirekodi nyimbo nyingi zilizopendwa na jamii ya watanzania.

Mapya yaibuka Afrika Kusini baada ya kugundulika kuwa M 2 the P hajafa, juhudi za kuuleta mwili wa Ngwea zaendelea kushika kasiNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HABARI mpya juu ya tukio la msiba wa Albert Mangwea zinaendelea nchini Afrika Kusini, huku habari zikikanusha kifo cha msanii mwingine aliyekuwa na Ngwea, anayejulikana kwa jina la M 2 the P.


Ngwea kushoto na M 2 the P walipokuwa nchini Afrika Kusini.
Taarifa hizo zinaonyesha kuwa msanii huyo hajafa, huku juhudi zinazofanywa kwa sasa ni kufanikisha kuuleta mwili wa Mangwea. Msiba wa Ngwea kwa sasa upo nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Ngwea atazikwa nyumbani kwa mama yake mkoani Morogoro na harakati za wadau zinafanywa ili kupata fedha za kugharamia kuletwa kwa mwili wa msanii huyo aliyefanya vyema katika tasnia ya Bongo Fleva, kabla ya kifo chake.


Albert Mangwea aliariki Dunia nchini Afrika Kusini katika Hospitali ya Helen Joseph ya jijini Johanesburg alipopelekwa baada ya kugunduliwa na wenzake asubuhi kwamba alikuwa hoi.
Hali hiyo ilimkuta maeneo ya Brixton-Mayfair West ambapo alikuwa amefikia kwa rafiki yake ambaye walisoma wote miaka ya nyuma.

Msiba wa Ofisa Habari wa Bunge, Ernest Zulu wazua utata, ndugu waanza kuvutana kabla ya maziko yake


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI ha hatari imejitokeza katika msiba wa Ofisa Habari wa Bunge, Ernest Zulu, baada ya jana usiku kutokea mvutano kutokana na upande mmoja kalazimisha aende kuzikwa kwao Songea, huku watoto wakitaka azikwe jijini Dar es Salaam.
Marehemu Ernest Zulu kulia enzi za uhai wake.
Kabla ya kifo chake, marehemu alitoa usia kuwa akifa basi azikwe jijini Dar es Salaam alipozikwa motto wake wa kwanza, hata hivyo kaka wa marehemu, Emmanuel Zulu, amekuja juu akitaka mdogo wake akazikwe nyumbani kwao.

Kifo cha Mangwea chatikisa nchi, mipango ya kuleta mwili wake yawekwa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAJONZI. Kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa nchini Afrika Kusini, Albert Mangwea, kimeendelea kutikisa vichwa vya watu wengi hapa nchini, huku Shirikisho la Muziki Tanzania likitoa tamko kwa mara ya kwanza.


Mangwea enzi za uhai wake
Wasanii mbalimbali, akiwamo Mrisho Mpoto, Afande Sele na wadau wengine kila mmoja anaelezea kwa mtazamo wake kifo cha Ngwea kilichotikisa hisia zao.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...