Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa
benchi la ufundi laa timu ya Coastal Union, ambaye pia ni mdhamini wa klabu
hiyo, Nassoro Binslum, amesema klabu za Simba na Yanga zina mtaji mkubwa wa wanachama wenye nazo, ila zinashangaza pale zinapokosa maendeleo ya soka la Kimataifa.
Nassor Ahmed Binslum
Coastal
imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya sita, huku ikipania kujiwekea mikakati
kabambe kwa ajili ya kuiongoza timu yao, hasa kwa kuwasajili Haruna Moshi Boban
na Juma Nyosso, wote kutoka katika timu ya Simba.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Bin Slum, alisema kwamba Simba na Yanga zimesheheni
wanachama na wapenzi wa kila aina, wakiwapo viongozi wa serikali na wafanya
biadhara wenye nazo.
Alisema
kwasababu hiyo, wana kila sababu ya kujiendesha kimataifa, hasa kwa kucheza
soka lenye ubora sambamba na kuwania mataji makubwa duniani ngazi ya klabu.
“Nashangaa
kwanini hizi klabu hazina maendeleo wakati zina mtaji mkubwa wa wanachama na
wapenzi ambao wengi wao wana nafasi kubwa, hivyo huu ni udhaifu wa aina yake.
“Nafasi
waliyokuwa nayo hawa wanaoitwa wakongwe, endapo wangeipata watu kama sisi, hakika
tungevuka malengo ya timu ya TP Mazembe, ambayo leo imekuwa tishio Afrika,”
alisema Bin Slum.
Bin Slum
ni miongoni mwa wadau wa mpira wa miguu wanaojipambanua vilivyo kuhakikisha
kuwa mkoa wa Tanga unarudi kwenye chati zake kwa kuhakikisha kuwa Coastal Union
inatamba ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment