Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Morogoro
GWIJI wa muziki wa Hip Hop
nchini, Selemani Msindi, maarufu kama Afande Sele, amesema mkoa wao Morogoro
umepata heshima kubwa, kutokana na kukusanya wasanii wenye uwezo wa aina yake.
Afande Sele akizungumza jambo katika kumuaga marehemu Albert Mangweha Ngwair mkoani Morogoro wiki iliyopita.
Afande Sele aliyasema hayo
mjini Morogoro katika mazishi ya msanii Albert Mangweha Ngwair, yaliyofanyika
katika Makaburi ya Kihonda Kanisani na kujaza watu wengi na kushangaza umma wa
Watanzania.
Akizungumza na Handeni Kwetu mkoani Morogoro, Afande
Sele, alisema Morogoro imejaa wasanii, akiwamo Ngwair ambaye kifo chake
kimetokea akiwa nje ya nchi akitafuta maisha kwa kupitia sanaa yake.
Alisema kuwa wanaamini wakazi
wote wa Morogoro na Watanzania kwa ujumla wataendelea kuusapoti muziki wa
Tanzania, kwa ajili ya kuwasaidia wasanii, akiwamo Ngwair ambaye kwa sasa ni
marehemu.
“Tunalia kwasababu tumepoteza
msanii mwenzetu, aliyekuwa na uwezo wa juu kwa namna moja ama nyingine, huku tukiamini
kuwa pengo lake haliwezi kuzibwa kirahisi kutokana na umahiri wake.
“Alikuwa ni msanii mwenzetu,
huku akiwa ni mkazi wa Morogoro, kwasababu maisha yake kwa kiasi kikubwa
ameyatumia mkoani Moro, hivyo tutaendelea kumuombea kheri na Baraka tele,” alisema
Afanden Sele.
Msanii huyo ni miongoni mwa
watu wanaokubalika mno mkoani Morogoro, akiitumia vyema nafasi yake ya
kujichanganya na jamii kwa kupitia tasnia ya muziki wa Hip Hop nchini.
No comments:
Post a Comment