Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SERIKALI imesema
italiangalia upya suala la vilabu vya soka vya Tanzania vya Simba, Yanga na
Falcon kwenda nchini Sudan kushiriki katika michuano ya Kombe la Kagame ambayo
inaandaliwa na Baraza la Michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na
Kati-CECAFA.
Bernad Membe, Waziri wa Mambo ya Nje
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Bernand Membe kuulizwa juu ya usalama wa timu hizo zitakapokwenda
jijini Darfur ambako michuano hiyo imeandaliwa.
Membe amesema mpaka sasa
hali ya kiusalama katika mji huo bado haijakaa vizuri kwani wageni wote
wanaofika huko hupokelewa kwa magari maalumu ya kuzuia risasi pamoja na nguo
ngumu za kuzuia risasi.
Waziri huyo aliendelea kusema kuwa pia hakuna
hoteli nzuri na zenye usalama na kuonyesha kushangazwa na watu waliokubali
michuano hiyo ifanyike huko wakati wanajua hali ya kiusalama sio shwari.
Membe
amesema kama wizara kwa kushirikiana na vyombo vinavyohusika vitatoa taarifa za
awali kabla ya hawajatoa mapendekezo kinyume chake ili kuzuia uwezekano wa
kuzitosa timu zetu sehemu ambayo inaweza kuhatarisha usalama wao.
Michuano
ya Kagame safari hii imepangwa kufanyika katika miji ya Darfur ya Kaskazini
pamoja na Gordofan ya Kusini Kuanzia Juni 18 mpaka Julai 2 mwaka huu ambapo
kutakuwa na makundi matatu huku Kundi A likiwa na timu za Merreikh-Elfasher ya
Sudan, APR ya Rwanda, Simba ya Tanzania na Elman ya Somalia.
Wakati kundi
B litakuwa na timu za Al-Hilal-Kaduugle ya Sudan, Tusker ya Kenya, Al Nasir ya
Sudan Kusini, Falcon ya Zanzibar na Al Ahly Shandi ya sudan huku kundi C likiwa
na timu za Yanga ya Tanzania, Express ya Uganda, Ports ya Djibouti na Vital O
ya Burundi
No comments:
Post a Comment