Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
HABARI ambazo hazijathibitishwa rasmi zinasema kuwa mume wa mwimbaji
mahiri wa taarabu, akiwa ndani ya kundi zima la TOT, Khadija Kopa, Jaffari Ally
amefariki Dunia, katika Hospitali ya Lugalo.
Habari ambazo
hazijathibitishwa na ndugu wa marehemu, akiwamo mke wake Khadija Kopa, zinasema
kuwa marehemu Ally alipelekwa Hospitalini hapo siku ya Jumatatau kwa ajili ya
kupata matibabu.
Taarifa za msiba huu
zinaendelea kufuatiliwa na kuandikwa kwa urefu zaidi.
No comments:
Post a Comment