Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Morogoro
MBUNGE wa Mbeya Mjini kwa
tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi, maarufu
kama ‘Sugu’ amewataka wasanii wasibweteke na umaarufu wanaopata, hasa katika
vifo vyao, wakati wanaishi maisha magumu.
Mbunge Sugu alipomuaga marehemu Ngwair
Sugu aliyasema hayo alipokuwa
anazungumza na wakazi wa Morogoro na wageni waliokwenda kumuaga marehemu Abert
Mangweha ‘Ngwair’, aliyofariki Jumanne iliyopita, nchini Afrika Kusini.
Alisema kuwa Ngwar amefariki
Afrika Kusini akiwa katika mihangaiko, lakini maisha yake ni kama yaw engine,
maana wamekuwa wakiishi kwa tabu, licha ya kufanya kazi nzuri na kupendwa na
watu wengi.
Alisema jambo hilo ni
changamoto kubwa kwao, hivyo wasanii wote lazima wajipange kuendeleza harakati
kwa ajili ya maendeleo yao kwa ujumla, maana hali ya wasanii inazidi kuwa
mbaya.
“Wasanii tusidanganyike na hali
hii ya kujaza uwanja katika vifo vyetu, ila lazima tujuwe tatizo lipo wapi na
kufanya mambo makubwa, sambamba na kuizindua serikali yetu.
“Tunaamini kwa pamoja, mambo
yatakuwa mazuri, hivyo huu ni wakati sasa wa kufanya kazi huku tunajua namna
gani tunaweza kujikomboa, maana umaarufu na vifo vya aina hii vyenye kujaza
watu wengi ni njia ya kuonyesha namna gani vijana tunakubalika,” alisema Sugu.
Sugu ni miongoni mwa wasanii
wanaokubalika mno katika tasnia ya muziki wa Hip Hop, ambaye kwa sasa
anaendeleza harakati zake hata baada ya kufanikiwa kuingia Bungeni,
akiwakilisha jimbo la Mbeya Mjini.
No comments:
Post a Comment