https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Friday, February 28, 2014

Kila la kheri Yanga kesho dhidi ya Al Ahly ya MisriNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kutoka Misri.

Mechi hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia 10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.

Maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.

Milango yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani (Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au vifaa vyovyote vya chuma.

Thursday, February 27, 2014

Pata picha tano kali za msanii Recho wa THT aliposherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuwakaribisha wakali kibao

 Msanii Recho wa THT kulia, akiwa kwenye picha wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, katika Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama.....

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam


MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Winfirda Josephat (Recho), mwishoni mwa wiki alifurahia siku yake ya kuzaliwa, huku akiahidi kufanya kazi nzuri zaidi kwa ajili ya kuonyesha makali yao kisanaa.Sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa mwanadada huyo ilifanyika katika Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wasanii wenzake.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Recho alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa kipaji kiasi cha kukitumikia kwa mafanikio.

 Unamjua Recho? Huyo hapo kushoto.
 Recho wa THT kushoto akishow love katika sherehe yake ya kuzaliwa mwishoni mwa wiki.

Diamond avunja ukimya juu ya watu wanaompikia majungu

Mbunge Masele awajengea uwezo mama lishe mkoani Shinyanga

 Mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Ndugu Stephen Masele akizungumza kwenye mkutano na wakina Mama na Baba Lishe wa Shinyanga mjini ambapo aliwasaidia kufungua SACCOS na kuwaongezea mtaji wa biashara yao.
 Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia jambo wakati wa hotuba ya Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
 Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia baada ya kuwezeshwa pesa kwenye mitaji ya biashara yao Mbunge wao Ndugu Stephen Masele, kwenye ukumbi wa  NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.

Wednesday, February 26, 2014

KWA niaba ya uongozi wa Coastal Union, tunatangaza msiba wa mchezaji wa zamani wa timu hii Bakari Jeki, pichani, aliefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya rufaa Bombo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kaka wa marehemu ndugu Ally Jeki, ndugu yetu aliugua kwa muda mfupi ambapo alilazwa katika hospitali ya Bombo wiki iliyopita mpaka mauti yalipomfika siku tatu baada ya kuanza kuugua.
Mwandisi wetu alizungumza na mchezaji wa zamani wa Coastal Union, ambae alipata bahati kumuona Bakari Jeki akiitumikia Coastal Union, Razak Yusuf ‘Careca’ ambae alibainisha kuwa marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika timu.

“Coastal Union imekosa mtu muhimu katika soka ambae alikuwa msaada mkubwa akitoa mawazo, vilevile alikuwa hakosi katika mechi na mazoezi ya timu,” Careca.
Aidha beki namba tano wa zamani Coastal Union, Mzee Salim Amir ambae alicheza na marehemu katika michuano ya UFUMA, iliyoandaliwa na Chama Cha Soka nchini (FAT), ambao ulikuwa ni ushauri wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere.

Nyerere alitoa ushauri huo ili kuisaidia FAT iliyokuwa chini ya Said El Maamry, kuondokana na madeni. Michuano hiyo ikapewa jina la Operesheni Futa Madeni (OFUMA).
Ilishirikisha timu nne ambazo ni Simba (Dar es Salaam), Nyota (Mtwara), Coastal Union (Tanga) na Nyota Afrika (Morogoro), Coastal Union waliibuka mabingwa marehemu Bakari Jeki akiwa beki mbili na langoni alikuwa mdogo wake Said Jeki ambae pia alikuwa golikipa wa Taifa Stars.

Twanga Pepeta kusugua kisigino CheetozNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya The African Stars, Twanga Pepeta, leo inafanya shoo ya aina yake katika Ukumbi wa Cheetoz, uliopo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, alisema kuwa onyesho hilo litakuwa la aina yake, kutokana na mikakati yao.
Alisema kuwa wadau wao wataendelea kupata burudani kali kutoka kwao ili waendelee kushika usukani katika tasnia ya muziki wa dansi.
“Tumejipanga imara kuhakikisha kuwa wadau na mashabiki wetu wanapata shoo za aina yake kutoka kwetu na kuonyesha makali yetu.
“Twanga haina mpinzani na ndio bendi yenye shoo nyingi kwa wiki, ikiwamo ya Jumatano ambayo sasa tutakuwapo Cheetoz ili kufanya mambo ya maana kwenye muziki wa dansi,” alisema.
Twanga Pepeta ni miongoni mwa bendi zenye mashabiki wengi hapa nchini, huku ikijihakikishia kuwa na shoo nyingi kuanzia Jumatano hadi Jumapili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe awasili nchini China

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)  akipokelewa na mwenyeji wake Mhe. wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China mara baada ya kuwasili kwenye  Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Na Mwandishi Wetu, Beijing, China
MHE. BERNARD K. MEMBE (MB.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amewasili nchini China tarehe 24 Februari 2014 nchini China kwa ziara ya siku tano, na kulakiwa na Bi. Sun Baohong, Makamu Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje China. 
Baada ya kuwasili Mhe. Membe alipokea taarifa ya maendeleo ya shuguli za ubalozi kutoka kwa Lt. Jen. (Mstaafu) Abdulrahaman Shimbo, Balozi wa Tanzania hapa China ambapo pia iligusia maeneo ambayo Mhe. Waziri atayatembelea yaani Shenzhen na Guangzhou.
 Mhe. Membe na Mhe. Wang Yi katika picha ya pamoja.
  Mhe. Membe akiongozana na Mhe. Wang Yi mara baada ya kupokelewa.

Bilioni 2.4 zahitajika kukarabati miundo mbinu ya shule ya sekondari Tanga School


(Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake)
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
JUMLA ya sh. Bilioni 2.4 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari ya Tanga School iliyopo mkoani Tanga kutokana na uchakavu ilionao baadhi ya majengo kwenye shule hiyo.

Shule hiyo inahitaji ukarabati wa miundombinu iliyokuwepo tokea mwaka 1967 ikiwemo madarasa,maabara,karakana, maktaba, mabweni,bwalo na zahanati ambazo ukarabati huo utaifanya kuonekana na muonekano mpya.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema maeneo mengine yanayohitajika ukarabati ni viwanja vya michezo,nyumba za walimu, Jengo la Utawala, Chumba cha Kompyuta na duka na Mgahawa wa shule pamoja na gari la shule.

Tuesday, February 25, 2014

Uingereza waanza chokochoko baada ya Uganda kuwabana mashoga nchini humo

Na BBC, Uganda
Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

 John Kerry asema Uganda inakiuka haki za binaadamu
Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema tangu Uganda iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita, Marekani ilieleza wazi kwamba sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha kuwepo haki za binaadamu ambalo tume ya haki za binaadamu Uganda inatambua linaambatana na sheria ya Uganda.
 
Kerry amesema,' Baada ya kuidhinishwa sheria hii, tunaanza ukaguzi wa ndani wa uhusiano wetu na serikali ya Uganda, kuhakikisha kwamba pande zote za uhusiano wetu, ukiwemo miradi ya msaada, zinapinga sera na sheria zinazowaonea watu na tuwe na uhusiano unaodhihirisha maadili yetu'.

Tamko hilo limetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kukaidi shinikizo la kimataifa na kutia saini sheria hiyo iliyo zusha mzozo, inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja Uganda, hatua iliyozusha hisia kali.


Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.


Marekani inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake na kutishia jamii ya wapenzi wa jinsia moja Uganda.
HABARI HII IMEKUJIA KWA HISANI YA BBC

Dkt Salim Ahmed Salim ndio kijana mdogo zaidi aliyewahi kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania, Jamhuri ya Uarabu ya Misri

Dkt Salim Ahmed Salim pichani kushoto akiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, enzi za uhai wake.

JE WAJUA?
DKT SALIM AHMED SALIM NDIYE KIJANA MDOGO ZAIDI KUWAHI KUTEULIWA KUWA BALOZI WA TANZANIA.

Mara baada ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo mwaka 1964, Mambo ya Nje ni moja ya mambo yaliyokubalianwa kuwa yawe ya Muungano, hivyo nafasi kama za Ubalozi katika Nchi mbalimbali Washirika na Taasisi za Kimataifa ilibidi zigawanywe kati ya Watanganyika na Wazanzibari ili dhana ya Utanzania ipate kuonekana dhahiri.

Ni katika wakati husika ndipo Rais Julius Nyerere, Kama Mkuu wa Nchi na mtu mwenye Mamlaka ya Uteuzi wa Mabalaozi alipoomba majina ya wale ambao walionekana kuwa na sifa za kuteuliwa kuwa Mabalozi kutoka Zanzibar kwa Rais Abeid Amani Karume.

Miongoni mwa majina yaliyoletwa na Sheikh Karume kwa Mwalimu Nyerere ni jina la Kijana mdogo wa miaka 22 Salim Ahmed Salim, jambo ambalo lilimfanya Mwalimu Nyerere amuulize mara ya pili Rais Karume juu ya umri wa Kijana huyo, majibu aliyopewa ni kuwa huyo ni Kijana wa Zanzibar mwenye vigezo na uwezo, apewe nafasi.

Wakulima wilayani Handeni waaswa kulima mazao ya biashara na chakulaNa Mwandishi Wetu, Handeni

WANANCHI wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameaswa kulima maza ya biashara na chakula ili kuwaondolea balaa la njaa linalowakumba kila mwaka kutokana na kutegemea kilimo cha aina moja, yakiwamo mahindi.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Muhingo Rweyemamu katika mahojiano maalum wilaya Handeni mkoani Tanga, ikiwa ni sera na mipango kabambe ya kuweka sawa jambo hilo kwa maendeleo ya wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla.


DC Muhingo alisema kuwa wakazi wengi wa Handeni wanategemea kilimo cha mahindi kama zao la biashara na chakula, jaambo linalowafanya kila wakati watu wengi wakabiliwe na njaa na kuwafanya waishi kwa tabu wakati wote.

“Ofisi yangu inajitahidi kuwaelimisha wananchi wengi waone ipo haja sasa ya kulima mazao mengi ya biashara, ukizingatia kuwa sasa wengi wao wanategemea mahindi kama zao la chakula na baadaye huuza kwa mahitaji yao.

“Naamini yapo mazao mengi ambayo endapo yatalimwa kwa wingi, mahindi yatahifadhiwa kwa ajili ya chakula wao na familia zao, maana suala la njaa Handeni linatokea kwasababu kuna mapungufu mengi, hasa ya chakula kuwa haba,” alisema.

Kwa mujibu wa Muhingo, elimu ya ziada kwa wananchi na wakulima wote kwa ujumla inahitajika wilayani humo ili watu wazoee kulima mazao mbalimbali, ukiwamo ufuta, maharage na mengineyo kwa ajili ya biashara na kuweka akiba ya chakula kwa zao la mahindi.

22 wa Taifa Stars watajwa kuwavaa Namibia Machi tano mwaka huu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia (Brave Warriors) itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.

Wachezaji walioitwa katika timu hiyo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki wa pembeni ni Edward Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu Shooting).

Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).

Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa kuondoka Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.

Wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi zao kumalizika.

Picha nzuri Rais Museven akisaini Muswada wa kupinga ushoga nchini Uganda

RAIS wa Uganda, Yower Museveni, akionyesha ujasiri wakati anasaini muswada wa kupinga ndoa za jinsia moja, ukiwamo Ushoga. Kwa kusaini kwake kama anavyoonekana pichani, sasa Uganda ushoga utakuwa umezikwa rasmi. Ukibainika utakuwa na kosa la jinai. Museveni amesaini muswada huo huku akibanwa na mataifa makubwa yanayojificha kwenye mgongo wa Haki za Binadamu.

Extra Bongo ilivyoweka historia katika uzinduzi wa 'Mtenda Akitendewa'Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi Extra Bongo Next Level wa zee wa Kimbembe juzi ilifanikiwa kukonga nyoyo za mamia ya mashabiki wa muziki wa dansi waliohudhuria uzinduzi waalbamu mpya ya bendi hiyo ya Mtenda Akitendewa uliofanyika kaika ukumbi wa DAR LIVE MBAGALA jijini Dar es Salaam.
Ally Choki wakati anazungumzia uzinduzi wao. Kushoto kwake ni Super Nyamwela na Ramadhan Masanja BanzaStone.
Kivutio kikubwa katika onyesho lilikuwa ni Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alipoingia ukumbini na gari la wagomnjwa Ambulance na kupanda jukwaani moja kwa moja kuanza kulishambulia jukwaa kwa wimbo uliobeba jina la albamu Mtenda Akitendewa.

Aidha mashabiki na wadau wa muziki wa dansi walionyesa kukunwa na ubora wa sauti za waimbaji wa bendi hiyo wakiongozwa na Choki, Banza Stone, Athanas Muntanabe na Richard Maarifa na Adam Bombole.Safu ya unenguaji ya bendi hiyo ikiongozwa na Super Nyamwela, Otilia Boniface ililishambulia jukwaa kwa shoo mpya ya Kimbembe na kuwafanya mashabiki wengi walihudhuria onyresho hilo kushindwa kutulia vitini hali iliyoleta msisimko mkubwa ukumbini hapo.

Katika onyesho hilo Extra ilisindikizwa na bendi ya Mashujaa ambayo nayoilifanya mambo sawasawa, huku pia malkia wa mipasho Khadija Kopa akinogesha uzinduzi huo.

 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Lina Sanga na Amin nao walikuwa sehemu ya burudani muhimu zilizopamba ukumbini hapo na kufanya onyesho kuacha midomo wazi wadau wa muziki waliofurika ukumbini hap

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...