Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora
waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa
mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo, huku mtaalamu wa uchekeshaji ambaye pia alishinda tuzo hiyo kwa mwaka huu, King Majuto akiwa kivutio kikubwa kwa wadau wa sanaa waliyohudhuria na kufuatilia kwenye vyombo vya habari hapa nchini.
Mzee King Majuto, akipokea tuzo ya mchekeshaji bora.
Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa
tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini
kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia
ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo.
Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin
Mangendela 'Stive Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi'
Nice Mohamed 'Mtunisi' Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike.
Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob
Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Iren Uwoya
na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda
'Jimmy Masta'.
Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent
Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu
mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri lakini
kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko 'Sajuki' John
Stefano,Hussein
Ramadhani Mkiety,'Sharo
Milionea'.
Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi.
No comments:
Post a Comment