Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU B ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga,
imeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Rolling Stone
yatakayofanyika jijini Arusha baadaye mwezi ujao.
Vijana wa timu B ya Coastal Union wakijinoa uwanjani.
Mashindano yaliyopita yalifanyika nchini Burundi, huku
vijana hao wakifanikiwa kushika nafasi ya pili na kulitangaza vyema Taifa
katika michuano ya vijana.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Meneja wa timu hiyo ya
vijana, Abdulrahaman Ubinde, alisema vijana wake wameanza mazoezi huku wakiwa
na malengo katika mashindano hayo.
Alisema timu yao ya vijana inafanya mazoezi kabambe kwa
ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya mashindano hayo ya Rolling Stone yenye
ushindani wa aina yake kwa mpira wa miguu.
“Tunatarajia uwezo wa kutosha katika mashindano hayo
ya Rolling Stone ambayo kwa hakika yamekuwa na ushindani wa aina yake, huku
mwaka jana tukishika naafsi ya pili.
“Vijana wapo Tanga wakiendelea na mazoezi makali kwa
ajili ya kujiandaa na mashindano haya, huku tukiamini kuwa mambo yetu yatakuwa
mazuri zaidi msimu huu,” alisema Ubinde.
Coastal Union ni miongoni mwa timu zenye malengo ya yake
katika mpira wa miguu, huku ikijipanga zaidi katika soka la vijana kama njia ya
kuzalisha wachezaji wenye uwezo wa kutosha.
Xxxx
No comments:
Post a Comment