Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UBAGUZI wa wasanii Tanzania umedhihirika leo baada ya
kususia msiba wa msanii mwenzao Hassan Kihiyo aliyezikwa saa kumi za jioni
katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni.
Jeneza la marehemu Kihiyo likiwasili eneo la makaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.Jeneza la marehemu Kihiyo likipelekwa kaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Jeneza la marehemu Kihiyo likipelekwa kaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Msiba huo ulihudhuriwa na wasanii wachache, hasa wale
wasiokuwa na majina makubwa, licha ya Kihiyo kujitoa mara kwa mara katika
matatizo ya wasanii wengine Tanzania.
Kihiyo alifariki jana jioni katika Hospitali ya Wilaya Temeke alipokuwa amelazwa akipata matibabu na kupeleka huzuni kubwa kwa baadhi ya wasanii na mashabiki wanaomuunga mkono.
Mazishi ya msanii huyu hayakuwa na tofauti na watu wengi, licha ya kucheza filamu kadhaa
na kushiriki kutengeneza movie za wasanii wengine kwa namna moja ama nyingine.
Kihiyo alicheza filamu zaidi ya nne, ikiwamo ile Mother House, Kaburi Moja,
Chanzo ni Mama, Where is God, My Book na nyinginezo.
Wadau na wasanii wachache waliohudhuria msiba huo ni pamoja
na Emmanuel Shija, John Mtitu, John Lister, mtunzi wa filamu na maigizo
Tanzania, Muddy Kimindu Kulinyangwa ambaye pia ametunga nyimbo mbalimbali za
taarabu kama vile Domo la Udaku la T-Moto Taarab, Nani Kama Mama wa Isha
Mashauzi na nyinginezo.
Mbali na kususia kwa wakali wa filamu Tanzania, mazishi ya
Kihiyo yalifanyika vizuri na kutanguliwa na swala, ambapo msikiti haukuwa mbali
na nyumbani ulipokuwapo msiba pamoja na sehemu ya makaburi aliyozikiwa
marehemu.
Wasanii wa Tanzania kwa mtindo huo wameonekana kubaguana
wenyewe kwa wenyewe, wakiangaliana usoni na wale wenye majina makubwa zaidi
ndio wanaoishi kwa kujuliana hali, hasa katika matukio ya misiba wakiamini
vyombo vya habari, wadau na mashabiki wataendelea kujazana kwa ajili ya kutaka
kuuza sura.
No comments:
Post a Comment