https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, October 31, 2016

Mkutano wa wadau wa pamba wafanyika mkoani Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akifungua Mkutano wa wadau wa pamba wenye dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha zao la Pamba katika mkoa wa Singida.
 Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida.

Serengeti waendelea kupokea madawati ya wahisani

Na Mwandishi Wetu, Serengeti
Mfuko wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda. Hii imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi.
“Tuko hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs Milioni 112 kwa Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.
Akipokea misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado zina uhaba wa madawati. 

Aidha Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo, nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.

Banda la Tanzania lang’ara maonyesho ya utalii nchini Saud Arabia

Na Mwandishi Wetu, Saud Arabia
MAONYESHO ya biashara na Utalii yaliyoandaliwa nchini Saud Arabia katika Mji wake Mkuu wa Riyadh, yamefanyika wiki iliyopita huku Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikionekana kung’ara baada ya wageni wengi kupendezwa na bidhaa zilizokuwa zinaonyeshwa katika banda la Tanzania.
Balozi Hemed Mgaza,  wakati anaapa baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia.
Katika maonyesho hayo ambayo bidhaa mbalimbali zilionyeshwa ukiwamo eneo maalum la mlima Kilimanjaro, nguo za Kitanzania na viatu pamoja na bidhaa nyingine muhimu zilizoonekana kuwapendeza wengi waliohudhuria maonyesho hayo.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza, alisema kwamba wananchi wengi waliohudhuria maonyesho hayo walionekana kuvutiwa zaidi na nchi ya Tanzania kutokana  na vivutio vyake.

Friday, October 28, 2016

Waziri asiyekuwa na wizara maalum Zanzibar akabidhi msaada wa matunda na vyakula

Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Mhe Juma Ali Khatib akikabidhi msaada wa Matunda na Vyakula kwa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar akipokea msaada huo Daktari Mkuu wa Hospitali hiyo Bi Zainab Kassim. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali hiyo huko Mental.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Mhe Juma Ali Khatib akisalimiana na Mgaga Mkuu wa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Bi Ruzuna Mohammed,wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa Matunda kwa ajili ya Wagonjwa wanaopata tiba katika hospitali hiyo. Kuu Zanzibar. 

CCM yawajia juu wanao kejeli utawala wa Rais Magufuli

Ndugu wanahabari,

Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeli, kudhihaki, kukatisha tamaa, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania.

Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu.

Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni Watanzania. Je ni tamaa ya madaraka tu au mengine? Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema kwa nchi.

Ndugu wanahabari,
Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita ya tathmini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Mamlaka ya maji safi Moshi yaongeza vyanzo viwili vya maji

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Prof Faustine Bee (kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge kuelekea katika chanz cha Mkashilingi kilichopo wilyani Hai kwa ajili ya uzinduzi, kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).Joyce Msiru.
Waziri wa Maji na Uwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanzo cha maji cha Mkashilingi kilichopo  wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Benki ya Posta yajenga choo cha Sh Milioni 14.5 jijini Tanga

 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Vyoo katika shule ya msingi Pande ambavyo limegharimu kiasi cha sh.milioni 14.5 kushoto ni Afisa Kilimo na Mazingira Jiji la Tanga,Ened Mzava na kulia ni Afisa Elimu Sayansi Kimu, Rukia Magogo 


 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses akizundua Jengo jipya la Choo cha Shule ya Msingi Pande ambalo wamelijenga.

Thursday, October 27, 2016

Wamiliki wa magari waombwa kuchukua tahadhari na wizi wa magari

RPC Suzan Kaganda

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

WAMILIKI wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili kuyanusuru kuibwa.


Mwito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Suzan Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni Innocent Dallu maeneo ya Mbezi Juu huku akiwemo mtoto wake Lightness.


"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wamiliki wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari ya kuzima magari yao na kufunga milango wanaposimama maeneo yoyote kupata mahitaji yao kwani si rahisi kumbaini mhalifu kwani wapo kila sehemu" alisema Kaganda.


Alisema katika tukio la kuibwa kwa gari la kampteni Dallu alikuwa amesimama maeneo ya Mbezi Juu bila ya kulizima akinunua mahitaji ambapo walitokea vijana wakaondoka na gari hilo aina ya Toyota Harrier baada ya kumtelemsha mmoja wa watoto aliyekuwemo ndani ya gari hilo aitwaye Philip huku wakiondoka na mdogo wake Lightness.


Alisema watuhumiwa hao walimtelekeza mtoto huyo maeneo ya Golden Bridge katika baa moja na kisha kuondoka na gari hilo ambalo lilipatikana baada kukamatwa na polisi Kiwangwa mkoani Pwani ambapo  kijana mmoja Ezekiel Daud anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.


Alisema ni vizuri wamiliki wa magari kuzingatia jambo hilo ili kuepusha matukio kama hayo ambayo yanapoteza muda mwingi wa kuyatafuta kwani tukio kama hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni ambapo wahalifu waliweza kuiba gari aina ya Noah lililosimamishwa bila ya kuzimwa na kuondoka nalo na alijapatikana mpaka leo hii.Matokeo ya Darasa la saba yatangazwa leo


Matokeo ya darasa la saba nchini Tanzania yametangazwa leo. Kupata matokeo hayo bonyeza chini

MATOKEO YA MITIHANI DARASA LA SABA 2016Jinsi ya kumpigia kura Karim Michuzi kushinda shindano la Airtel video


MPIGIE KURA KIJANA WETU KARIM MICHUZI ILI KUWEZESHA SHORT FILM YAKE YA "KA MBU" KUSHINDA SHINDANO LA AIRTEL VIDEO CHALLENGE. BONYEZA HAPA ILI UPIGE KURA...

Karola Kinasha aelezea tamasha lao la kukuza vipaji vya muziki

Baadhi ya Wasanii wa kundi la  Dar Creators
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwenye tamasha la muziki wa asili lililopewa jina ’Marahaba Swahili Music Festival’ lililofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Biafra na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Dar waliopata burudani mbalimbali za muziki wa ngoma za asili na nyimbo mbalimbali zilizoimbwa (Live).

Mmoja wa Waratibu wa tamasha hilo, Karola Kinasha alieleza lengo lake ni kukuza vipaji vya wasanii chipukizi wanaoimba na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki wa asili,na piia kuutangaza muziki wetu wa asili.

Wednesday, October 26, 2016

Tanzania yaadhimisha Siku ya Mtoto wa Kichwa Kikubwa

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi akifungua rasmi sherehe za kuadhimisha siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi Duniani,ambapo alisema wanakazi kubwa ya kutoa matibabu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na mifupa na mpaka sasa watoto takribani 202 wameshafanyiwa upasuaji na zoezi linaendelea Nchi nzima.
Mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Bw. Hakim ambaye nae mtoto wake anamatatizo kama hayo akielezea  kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa kuwa watu wengi wanahusisha tatizo hilo na imani potofu, aliongeza kuwa watoto waliofanyiwa upasuaji mkoa wa Mbeya ni 18, Morogoro 12, Mwanza 50, na Izazi 14. na wamefanikiwa kuokoa Maisha ya watoto 185 katika mikoa 16 Tanzania.

Bayport wanavyojivunia na huduma bora nchini Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Taasisi inayoongoza Tanzania kwa kubobea katika kutoa mikopo nafuu, Bayport Financial Services katika kipindi cha miaka 10  iliyopita  imechangia kwa kiwango kikubwa  katika kuboresha maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia  utoaji wa mikopo.
 Bayport Tanzania ni miongoni mwa taasisi tanzu kumi za Taasisi ya Bayport Group ambayo hutoa ufumbuzi wa kifedha  kwa watu binafsi walioko katika ajira rasmi au waliojiajiri ndani ya soko linaloibukia. Huduma zinazotolewa na taasisi hiyo  zinaboresha ujumuishwaji kifedha  kwa watu ambao hawana uwezo wa kuzifikia  huduma za kawaida za kibenki  au walio na kiasi kidogo cha fedha katika benki.
Baada ya kuanza shughuli zake  nchini Zambia mwaka 2001, shughuli za Bayport  kwa hivi sasa zinaendeshwa katika nchi saba barani Afrika na  nchi mbili ndani ya Amerika Kusini. Nchi hizo ni Zambia, Uganda, Ghana, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Msumbiji, Colombia, na Mexico.
 Hivi sasa Bayport  imekuwa ni msingi wa kuaminiwa na mteja ikiwa na  takribani wateja 518,000 ambao  kila mara wamekuwa wakipata  na hata na kufurahia huduma inazozitoa.  
 Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, Bayport imeshatoa  zaidi ya  shilingi bilioni 48 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015 peke yake. Kwa upande mwingine Bayport inachukuliwa kuwa ni ‘mlipa kodi mkubwa’  nchini Tanzania  ikiwa  imelipa  zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka wa fedha 2014.

Thursday, October 20, 2016

Shule ya Malangali mkoani Iringa yapata neema


Na Fredy Mgunda, Iringa

Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamewataka vingozi,wafanyabiashara, wakulima na wajasiliamali mbalimbali walinufaika na elimu kutoka shule ya malangali kurudisha fadhila katika shule hiyo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) alisema kuwa maendeleo aliyoyapata sasa ni kutoka na shule ya mangali hivyo ameamua kurudi na kuisadia shule hiyo. 

“Wafanyakazi na viongozi mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania.” Alisema Kevela
Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kuwasili katika shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania.

Mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Malangali na kuwaeleza jinsi gani shule hiyo ilivyowapa mafanikio hadi sasa walipofikia. 

Zoezi la kuchangia madawati jijini Tanga laendelea, Simba Cement wachangiadawati 1


Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement (Simba Cement), Dianna Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias  Mwailapwa, madawati 100 kwa  shule tatu za msingi, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba  za halmashauri ya jiji la Tanga kupunguza uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini.

KUFUATIA uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu. Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.

Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara  Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea chini kutoisha.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa, amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement)  na kuyataka mashirika na taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya wanafunzi kusomea chini.Kwa upande wake Afisa elimu shule ya msingi jiji , Khalifa Shemahonge, amesema madawati hayo yatatumika kama inavyokusudiwa na kuahidi kuyatunza ili kuongeza uelewa  wa  wanafunzi  darasani.   

Mapato yaongezeka wilayani Serengeti

Na Mwandishi Wetu, Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imefanikiwa kuongeza mapato yatokanayo na minada mbali mbali inayofanyika ndani ya Wilaya”

Hayo yamesemwa na Terry Hurson ambae ni Kaimu Mtunza Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti alipokuwa anazungumza na Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango waliofanya ziara katika Mnada wa Kijiji cha Rung’abure kilichopo Kata ya Rung’abure. 

Ziara hiyo ya ukaguzi ni mwendelezo wa taratibu zilizowekwa na Serikali kwa kuwahusisha Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kutembelea miradi kila baada ya miezi mitatu (Robo Mwaka wa Serikali)

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Porini Keya pamoja na Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Hamsini pamoja na wajumbe wa Kamati walijionea jinsi ukusanyaji wa mapato unavyofanyika kwa kutumia vifaa vya kieletroniki (POS) vinavyotumika pia kutoa risiti za malipo. “Mapato ya Minada yameongezeka kutokana na kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi na matumiz ya POS” alisema Terry Hurson. 

Ukusanyaji wa mapato unafanywa na watumishi wa Serikali, hii ni baada ya Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzitaka Halmashauri zote nchini kukusanya mapato na kuacha kutumia wazabuni katika kukusanya mapato kwenye masoko na minada.

Wachezaji watatu wa golf waitwa kuunda Timu ya Taifa

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Wachezaji Watatu wa Timu ya  Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya mchezo huo ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa klabu hiyo miaka 10 iliyopita kupata idadi hiyo.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Jijini Dar es Salaam nahodha wa Klabu hiyo ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema hatua hiyo ya furaha kwa klabu yao  imekuja baada ya mashindano ya wazi ya Arusha Open yaliyomalizika hivi karibuni Jijini Arusha.
Mchezaji wa Golf wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Michael Obare ambaye ameteuliwa kujiunga na Timu ya taifa akiwa kwenye harakati za Mcheo huo hivi karibuni Jijini Arusha.  Picha na Luteni  Selemani Semunyu.

”Ni mara ya kwanza na imekuja Muda Mchache baada ya klabu kupata Mwenyekiti mpya Brigedia Jenerali Michael Luwongo pengine ni ishara njema ya Uongozi wake katika klabu hiyo yenye malengo makubwa ya kubor eshwa.”  Alisema Masai.

Aliongeza kuwa Klabu hiyo iliwahi kutoa Mchezaji Mmoka Mwaka 2012 sasa hii ni kwa mara ya kwanza kwa Klabu hiyo kutoa Wachezaji wa Timu ya Taifa zaidi ya mmoja tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo Miaka 10 iliyopita na kutoa mchezaji hata mmoja Tangu Mwaka 2012.

Airtel yazindua “Airtel SimuBima” kuwezesha wateja kupata fidia za simu zao nchini.


Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari kusiana na huduma mpya ya linda simu ya Airtel Simu Bima itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money, kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Moses Alphonce na kushoto ni Muwakilishi wa shirika la Bima la UAP bw, Charles Matondane.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya UAP jana wamezindua huduma kabambe itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money.
Huduma hiyo mpya nchini kwa watumiaji wa smartphone itajulikana kama “Airtel SimuBima” ambapo itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbandoalisema “Leo Airtel tumeongeza sababu nyingine kwa wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu, sasa wateja wote wenye simu orijino za smartphone wataweza kusajiliwa na huduma ya Airtel SimuBima’ ambapo mteja mmoja anataweza kusajili hadi simu mbili  katika mfumo huu. Ikitokea mteja ameibiwa simu yake au kuipoteza basi kupitia huduma hii ya Airtel SimuBima’ tutampatia mteja huyo pesa ili aweze kununua simu nyingine atakayotaka na kisha simu iliyopotea itazimwa moja kwa moja isiweze kutumika tena”.
Meneja Masoko wa kampuni ya Bima ya UAP bw, Raymond Komanga akielezea jinsi mfumo wa malipo wa Airtel SimuBima unavyofanya kazi kwa kushirikiana  kampuni yake mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo ya kulinda simu za smartphone kupitia bima ijulikanayo kama Airtel SimuBima, katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money bw, Moses Alphonce (kulia) huduma ya AirtelSimuBima itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.
“Mteja wa Airtel ataweza kufaidi huduma ya “Airtel SimuBima” mara baada ya kupakuwa aplikesheni ya simuBima kutoka kwenye Playstore na kusajili taarifa za smartphone yake ikiwemo IMEI namba pamoja na gharama ya simu yake  na papohapo atapata ujumbe utakaomwambia gharama ya Bima ya simu hiyo kwa mwaka ambayo ataamua kuilipa yote au kuwa anailipa kwa kila mwezi” aliongeza Mmbando.

Saturday, October 15, 2016

Waaswa wasichaguwe kazi ili wafanikiwe kiuchumi

 Waumini wa Kanisa Katoliki wakiandamana wakati wa kuanza ibada ya Masista wa Jimbo la Dar es Salaam wa Shirika la Dada Wadogo la Mbagala Misheni baada ya kutembelewa na Umoja wa Wanaume wa Kanisa  Katoliki (Uwaka), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao jukumu lao kubwa ni kuwalea watawa hao.

Na Dotto Mwaibale

WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na kudharau kazi zingine kwani mbele za mungu kazi zote ni sawa na zinaheshimika.

Hayo yameelezwa na Monsinyori Padri Deogratius Mbiku katika ibada takatifu ya kuombea Umoja wa Wanaume Katoliki (Uwaka) kuwasaidia kwa hali na mali masista wa Shirika  la Dada Wadogo wanaoishi eneo la Mbagala Misheni jijini, Dares Salaam.

Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, alisema binadamu anapenda kuchagua kazi huku akionya kuwa watu waache kudharau kazi yoyote inayofanywa na mwingine ilimradi iwe ya halali.
Monsinyori Padri Deogratius Mbiku . wa Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (katikati), akiongoza ibada ya misa takatifu. Kushoto ni Padri Msaidizi wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph, Edward Sabbas na kulia ni Katibu wa Jimbo hilo, Aidan Mubezi.

CCM wamlilia mzee Tasili Mung'wenya aliyefariki mkoani Iringa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Abdulrahman Kinana ameitumia salamu za rambirambi familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Iringa Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda aliyefariki dunia jana tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga.

Mzee Mgoda amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TANU baadae CCM na Serikalini ambapo amekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafinga, Katibu wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkuu wa Wilaya Mstaafu.

Katika Salamu hizo Ndg Kinana amesema amepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa kifo cha Mzee Tasili Mgoda ambaye alikuwa ni sehemu ya hazina ya wazee wa CCM na kwamba anaungana na familia ya marehemu, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.

WanaCCM tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda. 
Amina

Wednesday, October 12, 2016

Msajili wa vyama vya siasa amuumbua Julius Mtatiro

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, amesisitiza kwamba ana mtambua Prof. Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho na Maalim Seif Sharrif Hamad kama katibu mkuu wa chama hicho.
''Mtatiro yeye ni nani, na ananipa Onyo kama Nani?, Ofisi ya Msajili inaitambua CUF moja tu, CUF ambayo mwenyekiti wake ni Lipumba na Katibu Mkuu wake ni Maalim Seif, Mtatiro hana mamlaka yoyote katika CUF kisheria hivyo asiendelee kuwapigia kelele''. alinukuliwa Msajili Mutungi.
''Chama cha siasa hakiwezi kuwa na uongozi wa aina mbili, yaani uongozi wa mwenyekiti Lipumba na Uongozi wa Mwenyekiti Mtatiro, hilo kwangu halitambuliki na halitakaa litambulike, lazima CUF waheshimu sheria za Nchi''. aliongeza Jaji Mutungi.
Kadharilka Msajili huyo amesema kwa sasa anaiona Bodi ya Wadhamini ya Chama hicho ikiwa imegawanyika makundi mawili, kundi linalomuunga mkono Lipumba na lile linalomuunga mkono Maalim.
''Anasema wadhamini, lakini anaonyesha wadhamini wawili tu, mwenyekiti na katibu, Bodi ya wadhamini ya CUF ni zaidi ya Mwenyekiti na Katibu, wapo wengine, na kwa kweli wamegawanyika kati kati wengine wameleta maombi haya, na wengine wameleta maombi yale, ofisi yangu haiwezi kuendeshwa na watu wa aina ya kina Mtatiro''. aliongeza
''Angewaambia waliosajiliwa Rita ni wangapi na hapo anao wangapi na msimamo wa wengine ni upi?, Ofisi yangu inawaheshimu wote 8 na haiwezi kufanya maamuzi kwa matakwa ya wajumbe wawili au watatu''. aliongeza
Aidha Msajili alisisitiza kuwa Ofisi yake ina wajibu wa kuhakikisha inasimamia fedha za umma ambazo zinatolewa kama ruzuku na kuhakikisha zinawafikia watu salama.
''Ruzuku ya CUF ipo salama na itaendelea kuwa Salama, walichoomba kina Lipumba ni kutambulishwa kama viongozi halali wa chama chao ili waweze kufungua akaunti, wala Msajili hajawatuma wakafungue akaunti ya Ruzuku, matumizi ya akaunti wanayajua waliofungua wenyewe''.. alisisitiza Msajili Mutungi.

Tabata waomba taka zilizotelekezwa mtaani kwao ziondolewe

Mchuuzi wa mbogamboga akipita karibu na takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na kituo cha daladala cha Tabata Kimanga mwisho Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
WANANCHI wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi mkazi wa eneo hilo, Mfaume Wakwetu alisema katika maeneo mengi ya Tabata Kimanga kunatakataka nyingi zimerundikwa kando ya barabara bila kuondolewa na wahusika.

Iringa nao wapigwa jeki ya madawati na mtandao wa Tigo

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akipokea madawati 85 kwa manispaa ya wilaya ya Iringa toka kwa Meneja wa Mauzo wa TIGO mkoa wa Iringa, Samwel Chamai kwenye hafla iliyofanyika ofisi za wilaya juzi.


Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiwa katika picha ya pamoja na meneja wa  mauzo ya tigo  mkoa wa iringa  Samwel Chamai na wanafunzi wa manispaa ya Iringa.

Tuesday, October 11, 2016

Tanzania yaanza kufanya utafiti wa mbegu za mahindi meupe

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda, akizindua utafiti huo katika Kituo cha Utafiti cha Makutupora mkoani Dodoma juzi.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
KWA mara ya kwanza Tanzania  imeanza kufanya utafiti wa mbegu ya mahindi meupe kwa kutumia teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) ambao utachukua takriban miaka mitatu ili kupata matokeo ya mbegu nzuri itakayostahimili mabadiliko ya hali ya hewa ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wakulima.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Hassan Mshinda alisema kuanza kwa utafiti huo ni hatua nzuri kwa nchi katika kuinua kilimo nchini.

Alisema utafiti huo ambao unafanyika katika nchi tano za Afrika, kwa hapa nchini unafanyika katika kituo cha Makutopora mkoani Dodoma na kuwa nchi hizo  nyingine ni Kenya, Uganda, Africa ya Kusini na Msumbiji. 
Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakiwa tayari kwa upandaji wa mbegu hizo katika Kituo cha Utafiti cha Makutopora mkoani Dodoma.

Shamba la mirungi lateketezwa kwa moto mkoani Kilimanjaro


Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu Uongozi wa Wilaya ya Same ulitangaza vita dhidi ya wakulima wa Bangi, na Mirungi huku akitangaza kuwa kifungo cha miaka 30 kitawahusu wakulima wote wanaojishughulisha na kilimo hicho haramu kwani Bangi na Mirungi ni hatari kwa afya za watumiaji na kuisababishia serikali hasara kwa kutopokea Kodi.

Kiama hicho kilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule wakati akikabidhiwa mradi wa Ruvu muungano uliojumuisha zahanati sita, Nyumba mbili za waganga, matanki saba ya kuvuna maji na madarasa 54, ofisi 16 za walimu, vyumba na vyoo vya chuo cha ufundi makanya uliofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania.
 Wakazi wa Kijiji cha Kisesa Kata ya Vudee wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa shambala Mirungi.

Siku ya SACCOS duniani yaadhimishwa jijini Dar es Salaam

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Saccos Duniani, Stellah Mtayabarwa (kushoto), akimwelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), alipotembelea banda la Saccos la Mamlaka ya Bandari (PTA), katika ufunguzi wa maadhimisho hayo uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard Kalinga (katikati), akihutubia wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo, Stellah Mtayabarwa.

LHRC waadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani

Ndugu wanahabari,

Leo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaungana na dunia nzima kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, siku ambayo ilipitishwa na  Umoja wa mataifa mnamo  Oktoba 11, 2011.  Kauli mbiu ya kitaifa kwa mwaka huu ni ‘‘Mimba na ndoa za Utotoni zinaepukika, Chukua hatua kumlinda mtoto wa kike’’. 


Hivyo basi katika kuadhimisha siku hii Kituo kimeangazia mtoto wa kike hapa Tanzania na changamoto anazokumbana nazo. Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, idadi ya watoto wa kike kati ya umri wa miaka 0-17 hapa Tanzania ni  11,263,891 idadi ambayo ni sawa na asilimia 48.8 ya watoto wote chini ya miaka 17, ambapo Tanzania bara  kuna watoto wa kike  elfu 10,943,846 na Tanzania visiwani idadi  yake ni laki 320,045. 


Hivyo basi nusu ya idadi hii ni wanawake na watoto  ikilinganishwa na idadi ya watanzania wote ambao ni milioni 44,928,923 ambapo  kati yao wanawake ni milioni 23,058,933. 

Inasikitisha kuona kuwa mtoto wa kike hapa nchini bado amekuwa akikabiliwa na changamoto nyingi na cha kusikitisha zaidi mtoto huyu anaanza kubaguliwa kuanzia katika ngazi ya familia. 

Katika familia nyingi za kitanzania mtoto wa kike amekuwa akikosa fursa ya kupata Elimu ukilinganisha na mtoto wa kiume na katika mazingira mengine wazazi wamediriki hata kuwaozesha watoto wao wa kike kwa ajili ya kupata fedha ya kusomesha watoto wa kiume. Ukiangalia pia katika suala zima la Elimu ni ukweli usiofichika kuwa idadi ya wasichana wanaoshindwa kumaliza masomo kwa sababu za kupata mimba imekuwa ikiongezeka.

Wazee wilayani Muheza wakumbukwa


 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza katika mdahalo wa siku ya wazee kiwilaya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazee Muheza.
Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (DAS) akizungumza neno kwenye kwenye mkutano huo.

Monday, October 10, 2016

Nishati ya umeme yafikia pazuri mkoani Tanga


MWENYEKITI wa mtaa wa Centrol Tanga, Diana Mussa, amewataka wakazi wa eneo hilo kuweka mazingira ya usafi kwa kila nyumba ili kuondosha kitisho cha magonjwa ya miripuko na kusema  kuwa  ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa duka la kuuza umeme la  Zola lililopo barabara ya Markert Street Tanga juzi , Diana amesema agizo hilo litakuwa endelevu na ofisi yake ikiongozwa na yeye kila siku asubuhi atafanya ukaguzi kwa kila mtaa.

Amesema halmashauri ya jiji imeweka vyombo maalumu vya kuhifadhia takataka na magari ya kusomba taka mtaani hivyo kutaka kila mmoja kuhakikisha eneo lake linakuwa katika mazingira mazuri. Akizungumza kwenye ufunguzi huo,Meneja mauzo kanda ya Kaskazini Tanga na Kilimanjaro, Peter Laizer, amewataka wajasiriamali wadogowadogo  kutumia umeme wa Zola na kusema  kuwa ni wa gharama nafuu.

Steve Nyerere aanza vizuri show yake Ukumbi wa Little Theatre

Mchekeshaji Steve Nyerere akitoa burudani katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria. Steve Nyerere amepanga kufanya onyesho la kuchekesha mara moja kwa kila mwezi ambapo mwezi ujao anatarajia kufanya onyesho hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Happi aalikuwa ni mmoja ya wageni waalikwa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alikuwa ni miongoni mwa wageni waliofika katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria.

Profesa Lipumba aanza ziara ya mikoa ya Kusini kwa mbwembwe lukuki

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameanza kufanya ziara za kukijenga chama chao akianzia na mikoa ya Kusini. Pichani juu ni moja ya tawi la Ngome Asili likizinduliwa leo na Lipumba. Picha kwa hisani ya CUF. 

Wadau waendelea kuipinga adhabu ya kifo Tanzania


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akisoma tamko la kupinga adhabu ya kifo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio na kushoto ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefungua kesi ya kikatiba kuhusiana na ulinzi wa haki ya kuishi na urekebishwaji wa sheria ya kanuni ya adhabu juu ya ulazima wa kutolewa kwa adhabu ya kifo katika makosa ya uhaini na mauaji.

Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali  wakitaka ufafanuzi zaidi juu ya adhabu ya kifo, wakibainisha kuwa adhabu hiyo haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi.
 Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Kituo hicho kimesema endapo Tanzania itatekeleza hukumu ya kifo  kwa sasa inamaanisha watu wapatao 228 na zaidi watapoteza maisha yao huku  wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.

Akizungumza wakati akitoa tamko la kupinga adhabu ya kifo  Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen- Kijo Bisimba alisema hadi  mwaka 2015 jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...