https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, June 20, 2013

Maandalizi ya Redd's Miss Kinondoni yazidi kupamba moto

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Hashimu Lundenga imetembelea kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 wanaotarajiwa  kumenyana leo alhamisi (leo) ya Juni 20 katika shindano Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiongea machache wakati kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont hoteli jijini Dar es Salaam. Kutoka upande wa mkuu wa Itifaki ni katibu Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta wakiwa pamoja muandaaji wa mashindano hayo Dennis Ssebo.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, akiongea na warembo wanaowania taji la Redds Miss Kinondoni 2013 mara baada ya kuwatembelea kambini kwao na kujua wanaendeleaje. Lundenga aliwaasa washiriki hao kuongeza bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika fainali yao.

Warembo wa Redds Miss Kinondoni wakiwa wamejipanga mara baada ya kumaliza mazoezi.
Akizungumza mratibu wa shindano hilo mara baada ya kuwakaribisha wageni, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...