Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na Wakuu wa
wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Mechi hiyo
itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za
ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina,
sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia
ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa
rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi
wabunge, ambao baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.
Alisema kuwa Watanzania
wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi
kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila
wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya wabunge.
“Tupo imara na
tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote
waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa
Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
“Katika mechi hizi,
mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa
Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen
Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.
Aliwataja Wakuu wa
wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto
(Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin Meela
(Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi
(Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda
(Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima
(Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha),
Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe),
uhingo rweyemamu handeni, Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi),
Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga
(Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji
wa timu hiyo.
Aidha, Muhingo
alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba
(Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni Mgaza
(Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula
(Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo)
Jacqueline Liana ( Magu).
No comments:
Post a Comment