MWILI wa marehemu Albert Mangwea, unawasili leo ukitokea nchini Afrika Kusini, Shirikisho la
Muziki Tanzania,
likitangaza kuwa kila kitu kinakwenda vizuri kwa
ajili ya kuuhifadhi kwenye nyumba ya milele.
Mwili wa Ngwea ukiwa tayari kwa kuagwa jana Afrika Kusini
Jeneza la NgweaNgwea
alifariki nchini Afrika Kusini Jumanne ya wiki iliyopita na kalenda ya uletwaji
wa mwili huo kuanza, hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa maziko yake.
Marehemu Ngwea enzi za uhai wake.
Mangwea akiletwa leo jioni, basi kesho Jumatano ataagwa katika viwanja
vya Leaders Club, wakati saa sita mchana safari ya kuelekea mkoani Morogoro
itaanza, huku mazishi yake yakipangwa kufanyika kesho au siku ya Alhamisi.
Akizungumza
na Handeni Kwetu Blog leo asubuhi, jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la
Muziki Tanzania,
Addo Novemba, alisema kuwa endapo mwili huo utafika leo Jumanne, basi maziko
yake yatafanyika siku ya Alhamis, Kihonda, mkoani Morogoro.
Aliwataka
Watanzania kuendelea kuwa wavumilivu katika msiba huo sambamba na kumuombea
marehemu aletwe Tanzania kwa
ajili ya kuzikwa katika ardhi ya nchi yao.
"Mara
kadhaa ujio wake umekuwa ukivunjika kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu, ila
tumehakikishiwa kuwa kesho leo Jumanne mwili wa ndugu yetu utawasili hapa
nchini.
"Akishaletwa leo, basi mwili wake utalala katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi
asubuhi ya siku ya Jumatano ambapo utaagwa mpaka mchana safari itakapoanza
kuelekea Kihonda, mkoani Morogoro, ambapo mazishi yake yatafanyika,” alisema
Novemba.
Msiba
wa Ngwea umepokewa kwa masikitiko makubwa, huku ripoti ya kifo chake ikishindwa
kuweka bayana, hivyo kuzua hofu miongoni mwa wadau na mashabiki wa muziki Tanzania.
Aidha, jana mwili huo uliagwa na Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini, hivyo kuonyesha kuwa uhakika wa leo kuletwa kwa marehemu ni mkubwa mno.
No comments:
Post a Comment