https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, July 30, 2017

Viane Kundi wa Iringa ajishindia Milioni 20 za Biko


*Issa naye achota Mil 10 zake
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imezidi kushika kasi baada ya droo yake ya 27 kutua kwa Viane Kundi wa mjini Iringa, nchini Tanzania aliyevuna jumla ya Sh Milioni 20, huku Ally Issa Kumburu mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam naye akivuna Sh Milioni 10 za Tamasha la Komaa Concert, lililofanyika jana na kudhaminiwa kwa kiasi kikubwa na Biko. 
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya Komaa Concert iliyorudiwa leo asubuhi baada ya jana kutopaatikana mshindi katika Tamasha la Komaa lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko Tanzania. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya 27 ya Biko ambapo Viane Kundi wa Iringa, alitangazwa mshindi na kuzoa Sh Milioni 20 za Biko. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda, akizungumza na wadau wa muziki waliofurika katika Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini mkubwa wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku'. Katika Tamasha hilo lililokwenda na kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 limempata Ally Issa Kumburu wa Mwananyamala, aliyepatikana katika droo iliyochezeshwa leo baada ya ndani ya tamasha kutopokea simu kutokana na wingi wa watu na kelele za uwanjani Tanganyika Packers, Kawe. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa EFM Radio, Denis Busurwa (Sebo). Picha na Mpigapicha Wetu.

Friday, July 28, 2017

Bagumako: Mamilioni ya Biko nimeyavulia kofia

Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 26 ya Biko, Leonard Bagumako wa pili kutoka kulia. Wengine pichani ni baba mlezi wa Bagumako, Gerlad Madaraka kushoto pamoja na mtumishi wa NMB, Tawi la Bank House, jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MSHINDI wa Sh Milioni 20 kutoka Bahati Nasibu ya Biko, Leonard Bagumako, amesema ameyavulia kofia mamilioni ya Biko, baada ya kukabidhiwa huku akiwa hakufahamu lolote kwamba yeye angeweza kuyatwaa.


Bagumako aliyasema hayo jana wakati anakabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 20, katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam, huku akiwa kijana mwenye umri wa miaka 21 tu anayefanya shughuli za uuzaji wa duka Kigamboni.

Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 26 ya Biko, Leonard Bagumako katikati. Kushoto ni baba mlezi wa Bagumako, Gerlad Madaraka. Picha na Mpigapicha wetu.


Akizungumzia fedha hizo, Bagumako alisema awali aliamini kuwa mchezo wa Biko unahusu watu matajiri, lakini baada ya kukabidhiwa fedha hizo, ameamini kila Mtanzania bila kuangalia wapi anaishi na uchumi wake anaweza kuibuka kidedea kwa kupata ushindi.


“Biko nimewavulia kofia kwa sababu kumbe hata sisi mafukara tunaweza kushinda zawadi mbalimbali za biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja za papo kwa hapo, bila kusahau ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kama niliyoupata mimi,” Alisema.

Wednesday, July 26, 2017

Leonard Bagumako wa Kigamboni akumbwa na Milioni 20 za Biko


Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki kushoto akiandika kumbukumbu muhimu baada ya kumpata mshindi wa droo ya 26 ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo Leonard Bagumako aliibuka kidedea kwa kujizolea Sh Milioni 20.  Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MFANYABIASHARA mdogo wa kuuza duka Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Leonard Bagumako, amekumbwa na mafuriko ya mamilioni kutoka bahati nasibu ya Biko, baada ya kutangazwa kushinda Sh Milioni 20 za droo ya 26 iliyochezeshwa leo.
Bagumako aliibuka kidedea ikiwa ni siku chache baada ya donge nono kama hilo katika droo ya 25 kwenda kwa Ally Hassan Lukinga wa Mtwara.

Akizungumza saa chache baada ya kupatikana mshindi huyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles, alimpongeza Bagumako kwa kuibuka mshindi kwenye droo hiyo ya aina yake, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa ya uwapo wa Biko kutajirika.

Alisema biko ni mchezo rahisi unaotoaa ushindi wa zawadi za fedha za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka Jumatano na Jumapili.

“Kila mtu anaweza kuibuka na shangwe kutoka Biko kwa kutwaa Sh Milioni 20, ambapo kucheza biko ni rahisi kwa sababu inachezwa kwa simu za mikononi ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa wachezaji kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea, ambapo Sh 1000 ina nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye kuwania sh Milioni 20, huku namba ya kampuni ya Biko ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.

Tuesday, July 25, 2017

Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko

Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven mwenye fulana ya Biko kushoto akiwa ameshika hundi saa chache kabla ya kumkabidhi kiasi cha fedha cha Sh Milioni 20 mshindi wa Mtwara, Ally Hassan Lukinga katikati. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, jana amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko, jumla ya Sh Milioni 20.


Makabidhiano hayo yamefanyika jana mkoani Mtwara katika benki ya NMB, ambapo Lukinga aliishukuru Biko na kusema kuwa fedha hizo atazitumia vizuri kuhakikisha zinakuza uchumi wake.


“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha hizi ambazo kwa hakika nitazitumia vizuri kama sehemu ya kupiga hatua kiuchumi kama dhamira ya Biko kuanzisha bahati nasibu yao.

Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko Tanzania, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia, akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa mjini Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyeshinda katika droo ya 24 Jumapili. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.

“Awali sikuamini kama naweza kushinda donge nono la Sh Milioni 20, hivyo ni wakati huu Watanzania wote kuamini kwamba Biko ni mchezo wa kubahatisha wa watu wote, maana kama hata mimi wa Mtwara nashinda, ndio kusema yoyote anaweza kushinda,” Alisema.

Sunday, July 23, 2017

Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara aibuka na Sh Milioni 20 za Biko


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko katika droo ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.


Lukinga fundi wa Tanesco alitangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed kushoto akiandika maelezo ya mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20 alilopata mfanyakazi wa TANESCO Mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga mara baada ya kupatikana kwenye droo ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja. Picha na Mpigapicha Wetu.
Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha pozi nzito baada ya kupatikana mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyetengazwa katika droo ya 25 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema ni mara ya kwanza kumpata mshindi wa droo kubwa ya Sh Milioni kutoka Mkoa wa Mtwara.


Alisema kupatikana kwa mshindi huyo kunaongeza wigo wa washindi wa Biko kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wanaoshinda droo kubwa pamoja na wanaoibuka na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

Wednesday, July 19, 2017

Milioni 20 za Biko zakimbiza homa ya Marianus wa Chanika


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ZAWADI nono ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, zimekimbiza homa ya mshindi wa droo ya 24 ya Biko, iliyotangazwa leo jijini Dar es Salaam, huku akiipata mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam, Enos Marianus.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza kwa simu na mshindi wa droo ya 24 ya Biko , Enos Marianus, aliyejizolea jumla ya Sh Milioni 20 atakazokabidhiwa haraka wiki hii. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed, akiandika dondoo za mshindi huyo wakati anazungumza kwa njia ya simu mara baada ya namba yake kuibuka kidedea katika droo hiyo ya 24. Picha na Mpigapicha Wetu.

Akizungumza kwa njia ya simu wakati anapewa taarifa za ushindi wake na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Marianus alisema kwamba amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku habari za ushindi wake zikiikimbiza homa iliyokuwa inamsumbua kwa wiki moja sasa.

Marianus alisema kwamba ushindi wa Sh Milioni 20 aliyotangazwa na Biko utakuwa muafaka kwake kutokana na kujihusisha na biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kusukuma mbele gudurumu la maisha yake.

“Nashukuru sana kwa kunitangaza mimi kuwa ni mshindi wa droo ya 24 ya Biko, hivyo hapa hata homa inayonisumbua imeondoka na nimepona kabisa kwa sababu ya habari zenu nzuri, nikiamini kwamba nikipata fedha hizo nitapiga hatua kubwa kiuchumi hususan katika biashara zangu,” Alisema Marianus.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba droo ya Jumatano imekwenda kwa mfanyabiashara mdogo wa Chanika, huku akiwataka wengine waendelee kucheza kwa ajili ya kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kwa Jumatano na Jumapili, pamoja na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Biko ni mchezo rahisi kushinda na unaweza kubadilisha maisha ya Watanzania, hivyo endeleeni kucheza kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku kiasi cha fedha cha Sh 1000 kikitoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa za Sh Milioni 20 za Jumatano na Jumapili, namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456,” Alisema.

Monday, July 17, 2017

Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
WITO umetolewa kwa washindi wa bahati nasibu ya Biko wanaoendelea kupatikana kila siku wafanye vitu vya maendeleo mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kulia akimkabidhi kiasi cha Sh Milioni 20 mshindi wao Fredy Nyari wa Kigamboni aliyeibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 katika droo ya 23 juzi. Kushoto ni Afisa wa NMB.

Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alipokuwa anamkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Jumadili (Jumapili), Fredy Nyari, akiwa ni mshindi wa droo ya 23 ya Biko.

Akizungumzia hatua ya makabidhiano ya fedha hizo, Heaven, alisema kwamba ikiwa siku zote mtu anakosa mtaji wa kuanzisha au kuendeleza biashara zake, kupata Milioni 20 kwa mara moja si jambo la mzaha.

Sunday, July 16, 2017

Fredy Nyari wa Kigamboni achomoza na Milioni 20 za Biko


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo amefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutesa hapa nchini.
Droo iliyompa ushindi mnono mkazi huyo wa Kigamboni maarufu kama ‘Jumadili’, imechezeshwa jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
Mwakilishyi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid kushoto akiandika dondoo muhimu katika droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku' leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Temeke, Fredy Nyari alifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko. Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
Picha na Mpigapicha Wetu.
Harakati za kumtafuta mshindi wa droo ya 23 Fredy Nyari wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, zilipofikia ukomo kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja kutoa neno kwa wadau na Watanzania kwa ujumla juu ya bahati nasibu ya Biko.

Akizungumza katika droo hiyo ya aina yake, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kumpata mshindi wao wa Kigamboni ni sehemu ya kuhakikisha kuwa washindi wao wanaendelea kuzoa mamilioni kutoka kwao baada ya kucheza Biko.
Alisema kila anayecheza Biko anasehemu kubwa ya kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo pamoja kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka katika droo kubwa za Jumatano na Jumapili.

Maeneo ya kuabudu Tanzania kuboreshwa


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora  Angela Kairuki akihutubia kwenye mkutano wa kitaifa wa shukrani na kumuombea Rais Dk.John Magufuli pamoja na nchi uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.

Kwaya ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama ikitoa burudani ya nyimbo za kumsifu mungu katika mkutano huo.

Friday, July 14, 2017

Mbunge wa Morogoro Mjini akabidhi milioni 20 za Biko kwa mshindi wao


Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MBUNGE wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, leo mjini hapa, amemkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Elizabeth Damian, aliyetangazwa mshindi katika droo ya 22 ya bahati nasibu hiyo inayojulikana pia kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyofanyika juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wa Biko Morogoro saa chache kabla ya kukabidhiwa fedha taslimu katika benki ya NMB, mjini hapa jana. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia.
 Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood wa tatu kutoka kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku, mshindi wa Morogoro Mjini, Elizabeth Damian wa pili kutoka kushoto. Wa kwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wakati wanamkabidhi mshindi huyo katika Tawi la benki ya NMB Morogoro jana.

Akizungumza katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 mjini Morogoro jana, Mbunge Abdulaziz, alisema bahati nasibu ni mchezo unaoweza kutoa fursa nzuri kiuchumi, huku akimtaka mshindi huyo azitumie vizuri pesa zake ili ziweze kumnufaisha kiuchumi.

Alisema kwamba jinsi mchezo wa Biko unavyochezeshwa ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba kila mtu anatumia vyema fursa ya kupiga hatua kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, hivyo wananchi wake wa Morogoro na Watanzania wote kwa ujumla waendelee kucheza ili wavune fedha za ushindi.

Wednesday, July 12, 2017

Milioni 20 za Biko zaenda Morogoro, Lohai naye avuta mkwanja wake



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

DROO ya 22 ya waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku, imefanyika leo jijini Dar es Salaam, huku mkazi wa Morogoro, Elizabeth Damian akifanikiwa kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 20 zinazotolewa na bahati nasibu hiyo.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Yassin Lohai akipiga picha ya shangwe baada ya kukabidhiwa fedha zake katika tawi la Madaraka la NMB jijini Tanga leo mchana. Lohai alikabidhiwa na Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven hayupo pichani.

Mwanadada huyo kutoka mkoani Morogoro, alitangazwa mshindi katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.


Akizungumza katika droo hiyo, Kajala aliwataka Watanzania kuendelea kucheza Biko ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kuvuna mamilioni yanayotolewa na Biko tangu kuanzishwa kwake, huku hadi sasa kwa miezi miwili ya Mei na Juni, zaidi ya Sh Bilioni moja zikienda kwa washindi.


Alisema fursa inayotolewa na Biko ni nzuri kwa uchumi wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba wanacheza Biko mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, sambamba dau nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili, kianzio cha kucheza kikiwa Sh 1000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ya Biko ikiwa ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

Tuesday, July 11, 2017

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Saba Saba jana

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, HE Hemed Mgaza, wa pili kutoka kulia, akiwa na mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya MIT Group of Companies kutoka Saud Arabia, Sameer Saleh Ahmed, wa pili kutoka kushoto wakiwa ndani ya banda la Kampuni ya Chai Bora kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mh Hemed Mgaza, akipata maelekezo yanayohusu utalii wa Tanzania kutoka kwa Aloyce Songay, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni Binafsi ya Hifadhi Mazingira Karatu (HIMAKA).

Sunday, July 09, 2017

Waziri Makyembe awa mgeni rasmi shindano la Bongo Style


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style, lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt. Mwakyembe.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu.

Biko yatoa Milioni 10 Tamasha la Komaa Concert la EFM Mwanza


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

DROO maalum ya kuwania Sh Milioni 10, iliyoandaliwa na waandaaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, imeenda kwa kijana mwenye miaka 25, Said Juma, mkazi wa Mwanza, ikitolewa katika tamasha la burudani la Komaa Concert la EFM Radio, lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa jana.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kushoto mwenye kipaza sauti, akimtangaza Said Juma kulia, aliyefanikiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 10 za Biko zilizotolewa maalum kwa ajili ya Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio Jumamosi iliyopita na kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Shabiki wa muziki wa kizazi kipya jijini Mwanza ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifuatilia onyesho la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko, ambapo pia alitafutwa mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko na Said Juma mkazi wa jijini Mwanza kuibuka kwenye droo hiyo maalum.

Katika tamasha hilo, wasanii mbalimbali wa jijini Mwanza na Dar es Salaam, walipata nafasi ya kutoa burudani kwa mashabiki wao, huku likinogeshwa na Milioni 10 za Biko maalum kwa wakazi wa Mwanza pekee.


Akizungumza katika droo hiyo ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo alipatikana kwa kupigiwa simu kama wanavyopatikana wengine waliowahi kuvuna mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu yao inayochezeshwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kupitia mitandao ya simu za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa.

Mbunge wa Kibaha Mjini afanya ziara ya kushutukiza eneo la ujenzi wa zahanati

 Na Ripota wa Mafoto Blog, Kibaha
MBUNGE wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka (kulia) na Diwani wa Kata ya Sofu, Yusuf Mbonde, wakishirikiana na wananchi wa kata hiyo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kusafisha eneo lililo na majani kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa Zahanati. Mhe. Mbunge jana asubuhi alifanya ziara ya kushitukiza katika eneo hilo baada ya kupata tetesi kuwa eneo hilo limeuzwa.

Aidha imeelezwa kuwa tetesi za kuuzwa kwa eneo hilo zilimfikia Diwani wa Kata hiyo, Bw.Mbonde, aliyeamua kumfuata Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kibaha, Jenifer Ommolo, ambaye 'eti' alikiri kuwa jambo hilo nalitambua na kumwahidi kuwa wangepewa eneo mbadala wa hilo, jambo ambalo Diwani hakukubaliana nalo na kuamua kulifikisha kwa Mbunge wake.

Friday, July 07, 2017

Tamasha la LABOR Day Marekani kurudishwa upya Septemba Mosi hadi tatu

Kama desturi ya Watanzania waishio Marekani hapo miaka ya nyuma kukutana wakati wa Labor Day Weekiend ndani ya Washington DC, sasa kuanzia mwaka huu wameamua kuirudisha upya desturi hiyo kwa kuandaa tamasha la aina yake likijumuisha michezo ya watoto, watu wazima, chakula pamoja na viburudisho mbalimbali vya wasanii kutoka Tanzania na Marekani. Habari kuhusu tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba Mosi hadi tatu mwaka huu, endelea kufuatilia vyombo mbalimbali vya habari ukiwamo Mtandao huu.

Lubeleje: Biko imeondoa changamoto zangu za kimaisha


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa droo ya 20 ya Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyofanyika Jumatano iliyopita, Philipo Lubeleje, amesema kwamba donge nono alilokabidhiwa na Biko limeondoa changamoto zake za kimaisha, kutokana na ugumu wa maisha anaokutana nao kwenye majukumu yake ya kila siku.
Mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Philipo Lubeleje, akiwa kwenye furaha baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 20 zakw kutoka wa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
 

Lubeleje anayejishughulisha na ujenzi wa nyumba jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha zake jana katika benki ya NMB jijini hapa, huku akisema amekuwa akiishi maisha magumu, hivyo anazitumia fedha zake vizuri ili akuze uchumi wake.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Lubeleje ambaye ni mkazi wa Gongolamboto, jijini Dar es Salaam, alisema amepokea ushindi wake kwa shangwe sambamba na kumshukuru Mungu kwa kumuona, akiamini kuwa amefanya hivyo baada ya kubaini kiu yake ya kupata maendeleo ya kiuchumi.

Wednesday, July 05, 2017

Rejesha ya wakazi wilayani Ubungo yaanzishwa


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali muda mchache mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM. Leo June 5, 2017

 Mfano wa Fomu ya huduma kwa mwananchi (Fomu ya malalamiko)

Mkutano wa Shukrani wa Kimataifa wakaribia


Phillip Luberege wa Dar es Salaam azoa Sh Milioni 20 za Biko

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
FUNDI ujenzi Phillip Luberege mwenye maskani yake Gongolamboto jijini Dar es Salaam, ametangazwa kuwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, akipatikana katika droo ya 20 ya kuwania Sh Milioni 20.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Gongolamboto, Phillip Luberege. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Kajala Masanja kulia akiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Luberege ametangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam katika droo ya 20 iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, akishirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo amepatikana baada ya kupatikana kwa washindi wa mikoani kiasi cha kuashiria kwamba kumekuwa na mwamko mkubwa kutoka kona zote za Tanzania kuchangamkia mchezo wao kwa watu kuchangamkia fursa ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

Tuesday, July 04, 2017

Maombi ya Kitaifa kufanyika Julai 13 hadi 15 mwaka huu


Mkuu wa wilaya Kibaha awapogeza washindi wa Biko


Na Mwandishi Wetu, Kibaha

MKUU wa Wilaya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama, amewapongeza washindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ na kuwataka kuweka umakini na malengo katika fedha zao wanazokabidhiwa ili wanufaike kiuchumi.

Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko, Goodhope Heaven kushoto akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Asumpter Mshama katikati wakati wa kumkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 19 ya Biko, Elisiana Laizer kulia mwenye gauni jekundu ndani ya benki ya NMB, Tawi la Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

DC Asumpter ameyasema hayo jana katika tawi la NMB, Mlandizi, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 zilizokabidhiwa kwa Mshindi wa droo ya 19, Elisiana Simon Laizer, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, mwenye maskani yake Mlandizi, aliyeibuka kidedea katika droo ya 19 ya bahati nasibu hiyo ya aina yake inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu za mikononi za Tigo, Vodacom na Airtel.


Akizungumzia bahati nasibu hiyo ya Biko, DC Mshama alisema michezo ya kubahatisha ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wao na uchumi wa Taifa kwa kuhakikisha kwamba wanafanya shughuli zenye kuleta maendeleo badala ya kuzitumia kwa mambo yasiyokuwa na msingi.

Sunday, July 02, 2017

Mjasiriamali Mlandizi mkoani Pwani azoa Milioni 20 za Biko

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, kushoto akizungumza jambo na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja katika kuchezesha droo ya 19 ya Biko ambapo mjasiriamali Elisiana Laizer kutoka Mlandizi, mkoani Pwani alifanikiwa kuwa mshindi wa Sh Milioni 20.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI mdogo wa Mlandizi, mkoani Pwani, Elisiana Laizer, leo  ametangazwa kuwa mshindi wa droo ya 19 ya kuwania Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutikisa hapa nchini.

Droo ya kumpata mwanadada huyo ilichezeshwa jana jijini Dar es Salaam na balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehus Ngolo.

Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba ni furaha yake kuona droo tatu kati ya 19 zilizoendeshwa na Biko zimewapata wanawake watatu, jambo linaloonyesha kwamba mchezo wao umekuwa wa Watanzania wote.

“Ni jambo la kutia moyo kuona droo ya 19 imempata dada wa Mlandizi, Elisiana ambaye anajishughulisha na biashara ndogo ndogo maeneo ya Mlandizi, mkoani Pwani, nikiamini kuwa ni hatua nzuri kwake na Kwa Watanzania wote wanaocheza Biko,” Alisema.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...