Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga anatarajia kuwa mgeni rasmi katika
ufungaji wa kozi ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) itakayofanyika
Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa kuanzia saa tano asubuhi.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Kozi hiyo iliyodumu kwa wiki nne,
ilifunguliwa rasmi Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo
Kurasini.
Mkurugenzi wa Ufundi Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Joseph Kanakamfumu, alisema Rais Tenga
ameridhia kufunga kozi hiyo baada kukosekana katika ufunguzi wa kozi hiyo
kutokana na majukumu aliyokuwa nayo.
“Kozi yetu ya ngazi ya pili itafungwa
Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa tano asubuhi na Rais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga ndiye atatufungia kozi yetu na
ameridhia kuwa atakuwa nasi,” alisema Kanakamfumu.
Alisema kozi hiyo itakuwa chachu ya
kupatikana kwa makocha watakaosaidia maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar
es Salaam na Taifa kwa ujumla.
Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA
tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya
Mwenyekiti Almas Kassongo.
No comments:
Post a Comment