Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KAMATI ya Utendaji ya
klabu ya Simba, leo jioni inatarajia kukutana kwa ajili ya kufanya kikao cha
kujadili mambo mbalimbali yanayohusu timu yao, ukiwapo mchakato wa usajili.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.
Simba inakutana huku
benchi la ufundi likihaha juu ya mlinda mlango wake, Juma Kaseja, ambaye
ameripotiwa kuwa huenda akawa nje ya timu hiyo kwa msimu mwingine wa ligi, japo
kocha wa Simba Mkuu, King Abdallah Kibadeni, ameonyesha nia ya kipa huyo abaki
kukipiga kwa msimu ujao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itangale maarufu kama
‘Mzee Kinesi’, alisema mambo yote yanayohusu klabu yao yatatangazwa kesho Ijumaa na kuiunda timu mpya ya ushindi.
“Kwa sasa hakuna
mwenye uwezo wa kusema lolote hadi kikao hiki kifanyike, hivyo hata kama hiyo
ripoti au mahitaji ya kocha ingekamilika, bado ingesubiri ridhaa ya Kamati ya
Utendaji.
“Kila kitu
kimekamilika kwa ajili ya kufanya kikao hicho, huku tukiamini kuwa siku
inayofuata, yani Ijumaa yatatangazwa maazimio yanayohusu mchakato mzima wa
Simba pamoja na usajili,” alisema.
Simba kwa sasa
inayonolewa na King Kibadeni, inafanya mazoezi yake katika Uwanja wa Kinesi,
Manzese, jijini Dar es Salaam huku wachezaji mbalimbali wakienda kwa ajili ya
kufanyiwa majaribio.
No comments:
Post a Comment