Na Mwandishi Wetu, Handeni
SERIKALI kwa kupitia Mkurugenzi wa Wilaya ya Handeni, Khalfany
Haule, imetangaza kupiga marufuku shughuli zote za uchimbaji au utafiti wa
madini, katika Mgodi wa Dhahabu uliopo wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Mgodi huo unaojulikana kama Magambazi, uliopo Magamba,
wilayani Handeni mkoani Tanga, umekuwa ukiibuka kwa matamshi ya kila aina, huku
ukikumbukwa pia kuleta mtifuano miongoni mwa wananchi wilayani humo.
Akizungumza mapema wiki hii, Haule alisema kuwa wilaya yao
imesimamisha shughuli zote zinazofanyika katika Mgodi huo, zikiwapo zile
zinazodaiwa kuwa ni kufanyika kwa utafiti juu ya dhahabu hizo.
Alisema yoyote atakayefanya kazi kinyume, atakuwa amekiuka
agizo halali, hivyo atalazimika kufanyiwa kazi, hivyo ni vyema wananchi na watu
wote wakafuata maagizo yao.
“Tumesimamisha shughuli zote zinazohusiana na mambo ya
dhahabu katika mgodi ule, hivyo kwa sasa hakuna atakayeruhusiwa kufanya jambo
lolote lile katika mgodi huo.
“Hata wale waliokuwa wakifanya utafiti hawataruhusiwa kwa
namna yoyote hadi hapo itakapotangazwa tena, maana kumekuwa na hila
inayofanyika, hasa madai kuwa wapo wanaochimba madini na kudai kuwa wanafanya
utafiti, hivyo kuleta mtazamo tofauti.
Kauli hiyo huenda ikazidisha au kupunguza ukakasi wa baadhi
ya wawekezaji katika migodi ya Tanzania wanaofanya shughuli hizo na kuliacha
Taifa katika mashimo na wao kunufaika.
No comments:
Post a Comment