https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, October 31, 2015

Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Moshi David Mosha atangaza kuachana na siasa

Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penfold kwa lengo la kuwashukuru wana CCM waliompigia kura.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.

Picha mbalimbali wakati Dr John Pombe Magufuli anakabidhiwa cheti cha Urais wa Tanzania

 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe. Anna Mghwira  na wagombea wengine wakiwa  katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais

Friday, October 30, 2015

Janet Mbene awashukuru wana Ileje kwa kumpa kura za kishindo Dkt John Magufuli

Na Mwandishi Wetu, Ileje
MBUNGE mteule katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe pichani, Janet Mbene (CCM) amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na  Dkt. Jonh Magufuli anayewania urais.
Akizungumza na wakazi wa Ileje, Mbene alisema ushindi wa kura 27,583 aliopewa na wana Ileje dhidi ya Emmanuel Mbuba wa NCCR Mageuzi aliyepata kura 14,578 atahakikisha anawapa wananchi hao kupitia ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakalibi.

“Awali ya yote niwashukuru wana Ileje kwa kuonesha imani kubwa kwangu, madiwani na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jonh Magufuli. Wana Ileje wametupa kura za kishindo nami ninawahaidi sitawaangusha katika utekelezaji wa ahadi nilizozitoa kwenu wakati wa kampeni,” alisema Mbene.

Mbunge huyo mteule alisema kuwa, kipaumbele chake cha kwanza  kitakuwa mindombinu ya barabara na kuwajengea uwezo wajasiriamali  ili kuzalisha bidhaa bora ikiwemo kuongeza thamani na mauzo. Mbene alisema, hatua hiyo itasaidia kuondoa umaskini wa kipato na msisitizo utakuwa kwenye ufugaji wa samaki, kuku, nyuki na mifugo yakisasa.

Pia alisema, kilimo nacho atakipa kipaumbele hususani cha alizeti, kunde, choroko, dengu, mbaazi,  soya , karanga  zikiwemo njugu mawe kwa wingi  kama mazao ya  iashara. “Nitahakikisha pia kilimo cha nafaka  ambacho kitahusisha mahidi,mpunga, ulezi , mtama na kilimo cha matunda aina mbalimbali yakiwemomananasi , maembe, maparachichi, mapera zikiwemo mbogamboga ilikuwainua wana Ileje kupitia kilimo chenye tija,” alisema Mbene.

Mbali na hayo alisema, kwa kushirikiana na wananchi ataibua vyanzo vya asili ambavyo ni vivutio vya watalii wilayani Ileje ili viweze kuwavutia watalii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.Pia alisema, atahakikisha anashirikiana na wananchi ili kuhakikishawanatatua kero mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na miundombinuhatua ambayo itasaidia kuinua vipato vyao, jimbo na taifa kwa ujumla.

Thursday, October 29, 2015

NMB Moshi watembelea Hospitali ya KCMC


Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB katika matawi ya Nelson Mandela na Mawenzi wakiwasili katika hosptali ya rufaa ya KCMC .

Wednesday, October 28, 2015

CCM yalalamika matokeo ya majimbo manne, yawashangaa UKAWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wana-CCM na kwa umma:

MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO
Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe. Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi. Kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya. Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa. Bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura. Hata hivyo, tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi, na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI

CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi. Tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru, uliofanyika kwa uwazi na kwa amani – na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa. Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC yasikitishwa na Maalim Seif kujitangaza mshindi wa urais Zanzibar

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema imesikitishwa na kitendo cha mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kujitangazia ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili tarehe 25 Oktoba, 2015 na imevitaka vyombo vinavyosimamia utii wa sheria kumchukulia hatua kiongozi huyo wa CUF.

“kitendo cha Maalim Seif kujitangaza mshindi amevunja kifungu cha 42 (5) cha sheria ya mwaka 1984 ambacho kinaipa mamlaka Tume ya Uchaguzi kuwa chombo pekee chenye mamlaka hayo” Mwenyekiti huyo alifafanua. Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo, Mweyekiti wa ZEC Jecha Salum Jecha alisema kuwa Maalim Seif ametenda kosa la jinai hivyo mamlaka zinazohusika zinapaswa kumchukulia hatua. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu akithibitika ametenda kosa hilo atahukumiwa kulipa faini ya Tzs laki tano au kwenda jela miaka mitano au adhabu zote.

“Tume haina mamlaka ya kumkamata wala kumhoji Maalim lakini viko vyombo vyenye mamlaka hayo hivyo itakuwa ni vyema vikatimiza wajibu wao kwa kumkamata na kumhoji mhusika hasa ukizingatiwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kutenda kosa kama hilo” Mwenyekiti wa Tume alieleza. Alibainisha kuwa Tume yake imekijadili kitendo hicho kwa makini na uzito unaostahiki na kubainisha kuwa tangazo hilo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini. Bwana Jecha alibainisha kuwa Maalim Seif, kama walivyo wagombea wengine 13 wa nafasi ya urais wa Zanzibar wanaelewa fika sheria hiyo hivyo alitoa wito kwa wagombea wengine kuwa watulivu kama walivyo wananchi.

Kuhusu kasi ndogo ya Tumeyake kutangaza matokeo, Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa kazi kubwa wanayoifanya ni kuhakiki kura kujua kama hakuna tofauti ya kura baina ya zile zilizoandikwa na hali halisi. “Wanaoandika na kuhesabu kura wote ni binadamu hivyo wanaweza kuchanganya mahesabu na ndio maana kazi yetu hivi sasa ni kulinganisha kura”alisisitiza Mwenyekiti wa Tume. Kuhusu kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura huko katika jimbo la uchaguzi la Chonga, Wilaya ya Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba, Bwana Jecha alikiri kutokea kwa hilo na kwamba suala hilo sasa liko chini ya mikono ya Jeshi la Polisi. Alitahadharisha juu vitendo vya baadhi ya wagombea kuchukua vyeti bandia vinavyoonesha kuwa tayari wao wameshinda nafasi za ubunge au ujumbe wa Baraza la Wawakilishi. Bwana Jecha alitoa wito kwa wananchi kufanya subira wakati huu Tume yake ikifanya kazi ya kukusanya na kuhakiki kura na baadae kuwatangaza washindi.

Sunday, October 25, 2015

Dk John Pombe Magufuli apiga kura wilayani Chato

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli akipiga kura yake jimboni kwake Chato mapema leo asubuhi Oktoba 25, 2015. (PICHA NA MWANDISHI WETU).

Kambi Mbwana akiwa kwenye foleni ya kupiga kura kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga

Mmiliki wa Mtandao huu na aliyekuwa mgombea ubunge katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kambi Mbwana, wa tatu kutoka kushoto, akiwa kwenye mstari wa upigaji wa kura katika Uchaguzi Mkuu, katika moja ya kituo kilichopo kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga leo Oktoba 25 kwa ajili ya kuchagua mbunge, diwani pamoja na rais. Picha kwa hisani ya group la HANDENI KWETU kwenye facebook.

Thursday, October 22, 2015

Dkt John Magufuli mgombea Urais wa CCM sasa kuomba kura kwa njia ya simu

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25 baada ya kubuni mkakati mpya wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura. 

Ujumbe huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais. Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa kuwa rais. Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani mkubwa.

Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi. Kutokana na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa awamu ya tano wa taifa hili. Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache zijazo.

Joyce Msiru ndio Mkurugenzi mpya wa mamlaka ya maji na mazingira Moshi


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi, MUWASA, Sharry Raymond akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wakati wa utamburisho wa Mkurugenzi mpya wa MUWSA. Picha zote na Dixon Busagaga 

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA.
Mwenyekiti wa Bodi ya MUWSA,akizungumza.

CCM kufunga kampeni kwa mtindo wa aina yake, Rais Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Kinana kufanya mashambulizi mikoani

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.

Kufunga Kampeni
CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo.  Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
 1.    Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
 2.    Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
 3.    Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
 4.    Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5.    Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6.    Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7.    Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu  Mstaafu
Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi saba.

Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.  Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

Makamu wa Rais Dkt Bilal aagana na watumishi wa ofisi yake

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewashukuru watumishi wa ofisi yake kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha miaka mitano kiasi cha kuweza kutekeleza majukumu ya msingi ya ofisi hiyo ya kudumisha Muungano na uhifadhi wa mazingira kwa ufanisi mkubwa.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Saz Salula, akizungumza kutoa shukurani wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya Mhe. Makamu wa Rais kuagana na Watumishi wa Ofisi yake. Hafla hiyo ilifanyika juzi Okt 20, 2015 kwenye Makazi ya Dkt. Bilal. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watumishi wa Ofisi yake (baadhi hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam, juzi Okt 20, 2015. Picha na OMR

Akizungumuza katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es salaam Dkt. Bilal alisema kuwa, anayo furaha kufikia kipindi hiki na kwamba alifanya majukumu yake vema kutokana na kuwa na wasaidizi mahiri na waliojitoa kufanya kazi zao kwa weledi na uvumilivu mkubwa muda wote.

“Natumia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote. Walinisaidia sana katika kipindi nikifanya kazi ya kuitumikia nchi yangu. Niwashukuru ninyi wafanyakazi wa ofisi yangu, mlifanya kazi kwa kujituma sana na majukumu yetu kwa mujibu wa taratibu tuliyatekeleza kwa ufanisi,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais na kuongeza:

“Nakutakieni kila la kheri katika utendaji wenu. Jitahidini kufanya kama mlivyofanya kwangu kwa yule atakayekuja baada yangu. Nakushukuruni kwa zawadi hasa ya vitabu maana mimi ni muumini wa kusoma, nitavisoma”. 

Wateja wa Bayport sasa kukopeshwa simu za mikononi

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani akizungumza jambo katika moja ya shughuli za taasisi hiyo nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SEKTA ya mawasiliano ni kati ya mambo muhimu na mazuri inayoweza kufanikisha kwa vitendo kukuza uchumi wa Taifa letu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kusimamia vyema sekta hiyo, uchumi wa Wwatanzania utakuwa kwa kasi.

Na katika mambo yaliyokuwa kwenye kundi hilo la mawasiliano, ni kuona Watanzania wanawasiliana kwa kumiliki simu imara ili waweze kuwasiliana katika mahitaji yao ya kimaisha, bila kusahau biashara na wajasiriamali.

Si lazima mtu aende mkoani Mbeya, Tanga, Arusha kufuata au kupeleka bidhaa zake bila kufanya uchunguzi swa soko, hususan kwa kuwasiliana na watu wanaoishi huko, au wale wanaoshirikiana katika majukumu yao ya kila siku.

Mke wa Dkt Shein achanja mbuga kumuombea kura mumewe visiwani Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Bububu kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi wa Wanawake wa Wilaya ya Mfenesini Unguja Kichama kuwaombea Kura Wagombea Wote wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Mfenesini Unguja Kichama akitowa salamu za Wilaya yake kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Bububu.
Viongozi wa UWT Wilaya ya Mfenesini Unguja wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kuwaomba kura kuwapigia Wagombea wote wa CCM.

Wednesday, October 21, 2015

SMZ yaipongeza UN kwa kuunga mkono juhudi za maendeleo Visiwani Zanzibar

IMG_9022
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (katikati) wakimkaribisha mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Picha na Zainul Mzige,

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema kuwa itaendelea kuthamini fursa mbali mbali zinazotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman wakati akihutubia katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar, alisema umoja huo umekuwa sekta muhimu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya serikali katika sekta mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Alisema kuwa Zanzibar ikiwa miongozi mwa nchi zinazoendelea barani Afrika inaendelea kutumia vizuri fursa zinazotolewa na umoja huo kwa lengo la kujenga jamii bora zenye kipato na uwezo wa kati kwa lengo la kupunguza umasikini nchini.

Dkt John Magufuli asafishiwa njia ya Ikulu

 
Kiongozi wa familia hiyo, Albert Michael, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geita.
---
Na Rashid Zahor, Geita.
FAMILIA ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli imesema Watanzania watakuwa na bahati ya kumpata kiongozi mchapakazi, mwenye msimamo na anayependa maendeleo. Imesema iwapo Dk. Magufuli atachaguliwa kuwa rais, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii, atawaletea maendeleo makubwa kwa kuwa ni mtu mwenye msimamo, asiyeyumba na anayependa maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na kiongozi wa familia hiyo, Albert Michael, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geita.
Mzee Albert hakuwepo Katoma juzi wakati msafara wa Dk. Magufuli uliposimama kwa muda nyumbani kwa babu yake, ambako alipata nafasi ya kuzuru kaburi lake na la bibi yake mzaa wa baba na kuwaombea dua. "Watanzania wasiwe na wasiwasi, Magufuli ni mtu anayependa watu na maendeleo na ni mchapakazi,"alisema Mzee Albert, alipokuwa akijibu swali kuhusu sifa za mgombea huyo tangu alipokuwa mtoto.
Aidha, Mzee Albert alisema Dk. Magufuli si mpole, sio mkali sana, lakini ni mtu mwenye msimamo na asiyeyumba katika jambo analotaka kulifanya. Mzee Albert, ambaye ndiye aliyeachiwa mji wa Katoma kwa sasa, liliko chimbuko la ukoo wa Dk Magufuli, akiwa miongoni mwa wadogo zake marehemu baba mzazi wa mgombea huyo, alisema familia yao ipo pamoja naye na inamuombea Mungu aweze kutimiza dhamira yake ya kuwa rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Ninachowahakikishia Watanzania ni kwamba Oktoba 25, watampata kiongozi bora, asiye na ubaguzi wa aina yoyote,"'alisema mzee huyo.

Tuesday, October 20, 2015

Dkt John Magufuli aendelea kufunika katika kampeni zake, jana atua mkoani Geita na kufanya mikutano katika wilaya mbalimbali mkoani humo

MGOMBEA urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kutokana na kukubalika kwake katika mikoa yote aliyokwenda kufanya mikutano ya kampeni, ana uhakika wa kupata ushindi wa tsunami katika uchaguzi wa mwaka huu. Amesema katika mikoa yote aliyokwenda kufanya kampeni, wananchi wamemkubali na kumuhakikishia kumpigia kura nyingi ili aweze kuwa Rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA.

Sunday, October 18, 2015

Makamu wa Rais Dkt. Bilal aweka jiwe la Msingi ujenzi wa vituo vya mradi wa mapumziko na vyoo vya wasafiriI katika barabara Kuu, kijiji cha Idetero,Mufindi, mkoani Iringa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, jana Okt 17, 2015. Picha na OMR
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mgimwa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, jana Okt 17, 2015. Picha na OMR

Dr John Magufuli alivyoshiriki kutoa heshima za mwisho msiba wa Deo Filikunjombe jana

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.PICHA NA MICHUZI JR.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.

Friday, October 16, 2015

Wengi wajitokeza kumzika Dr Abdallah Kigoda wilayani Handeni, mkoani Tanga


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo  nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji dada wa marehemu Dkt. Asha Kigoda  nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifarifi familia  nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba huo
 Spika Anne Makinda msibani hapo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa serikali na wa kidini   nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 akiongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili
 Bw. Saidi Yakub akiendesha shughuli hiyo
 Sehemu ya waombolezaji
 Sehemu ya waombolezaji
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Uledi Mussa akisoma wasifu wa marehemu

 Waombolezaji
 Sehemu ya waombolezaji
 Brigedia Jenerali Mstaafu  Ngwilizi akiongea machache kuhusu marehemu
 Rais Kikwete akipeana mikono na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema ZanzibarSalumu Mwalimu, ambaye aliwakilisha UKAWA kwenye mazishi hayo
 Ndg. Muhammad Seif Khatibu akisoma rambirambi za CCM 
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe akitoa rambirambi za serikali

 Waombolezaji kinamama msibani hapo
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally (mwenye kipaza sauti mkononi) akiongoza swala ya maiti
 Rais Kikwete akiwa anaongozana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman akitoa pole kwa waombolezaji
 Watumishi wa Bunge wakibeba jeneza lililo na mwili wa marehemu kuelekea kaburini
 Mazishi
 Mtoto wa marehemu akiweka udongo kaburini
 Rais Kikwete akiweka udongo kaburini 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman akiwa na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. John Kijazi kwenye mazishi hayo.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...