Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZEE wa Kisigino, bendi ya
African Stars “Twanga Pepeta” leo Jumapili inazindua albamu yake 10
ijulikanyo kwa jina la ‘Nyumbani ni Nyumbani’, katika Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni, sambamba na kusherehekea miaka 15 tangu kuanzishwa kwake.
Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu.
Uzinduzi huo utapambwa na
michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo timu nane za mpira wa miguu
zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano ijulikanalo kwa jina la ASET
Bonanza.
Timu hizo zitaongozwa na ile ya
waandishi wa habari za michezo, Taswa FC na nyingine kama Brake Point, Mango,
Namanga, Kivukoni, Camp Combine, Wagadau na Kunduchi.
Mbali a burudani kutoka kwa
Twanga Pepeta, siku hiyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wanamuziki wa
kizazi kipya, Linex, Barnaba, bila kusahau, wakongwe wa muziki wa dansi nchini,
bendi ya Mlimani Park maarufu kwa mtindo wa Sikinde Ngoma ya Ukae.
Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi
Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema kuwa kila kitu kimekamilika, huku akiamini
kuwa mashabiki wao watapataa kitu adimu kutoka kwao.
Alisema kuwa nyimbo zilizomo
kwenye albamu hiyo ni Nyumbani ni Nyumbani, Ngumu Kumeza, Mwenda Pole, Kila
Nifanyalo, Shamba la Twanga na Twanga 2013.
Albamu nyingine za bendi hiyo ni
Kisa Cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali Uzeeni
(2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004),
Safari (2005),Password (2006), Mtaa wa Kwanza (2007), Mwana Dar es
Salaam (2009) na Dunia Daraja iliyozinduliwa mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment