Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENKI ya CRDB imetangaza kuununua
wimbo uitwao ‘Fahari Huduma’ ulioimbwa na msanii Mataluma pamoja na taasisi ya
kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talents THT.
Mataluma wa THT akiwajibika jukwaani.
CRDB walitangaza uamuzi huo kupitia
kwa Mkurugenzi Mtendaji, Charles Kimei, katika uzinduzi wa huduma mpya ya benki
kwa kupitia mawakala itakayosambazwa nchi nzima kama sehemu ya kuwasogezea
Watanzania huduma za kuweka na kutoa pesa.
THT wakifanya manjonjo yao.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, kwenye uzinduzi huo, Kimei alisema amefurahishwa kwa jinsi wimbo huo
ulivyoimbwa na unavyochezwa, hivyo ameagiza watu wake wa masoko waununuwe
haraka iwezekanavyo ili usiweze kutumiwa na wengine.
Alisema kuwa endapo wimbo huo
hautanunuliwa, unaweza kutumiwa na makampuni mengine, wakati ni maalum kwa
ajili ya benki yao ya CRDB.
“Kwakweli nimefurahishwa kwa kiasi
kikubwa na wimbo huu, hivyo watu wangu wa masoko lazima make chini na taasisi
hii ili muununuwe ili usitumiwe tofauti na sisi CRDB.
“Unaweza kuitambulisha vyema huduma
yetu hii ya benki kwa njia ya wakala, ambapo mteja anaweza kutoa na kuweka
pesa, bila kusahau wale wanaolipa bili mbalimbali kwa kupitia mawakala wetu,”
alisema Kimei.
Huduma hiyo ya Fahari Huduma
inatarajiwa kupokewa vizuri na Watanzania, ukizingatia kuwa itakuwa
wamesogezewa karibu huduma za kibenki kwa njia ya mawakala badala ya matawi ya
benki, kama ilivyozoeleka wakati huu.
No comments:
Post a Comment