Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
TIMU ya Taifa, Taifa
Stars, leo inashuka katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kumenyana na timu ya Taifa ya Ivory Coast, katika mchezo wa kuwania kufuzu
Kombe la Dunia.
Mrisho Ngassa, mmoja wa nyota wa Stars.....
Stars inashuka
dimbani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa
Morocco, huku ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 6 nyuma ya Ivory Coast
yenye pointi 10, huku Morocco wakishika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi tano,
huku Gambia yenyewe ikibaki na pointi moja.
Mechi hiyo ni
mwendelezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, huku Stars ikiwa katika kundi C,
ambapo ina kila sababu ya kushinda leo dhidi ua Ivory Coast kaam inajitaji
kujieka katika mazingira mazuri ya kufuzu katika fainali hizo zinazotarajiwa
kufanyika mwaka 2014, nchini Brazil.
Timu ya
Taifa, Taifa Stars iliyoweka kambi yake katika Hoteli ya Tamfoma, bado ina
nafasi ya kuweza kufuzu kama itashinda katika michezo yake iliyosalia na kuwapa
raha Watanzania.
Mkuu wa
Mkoa Dar es Salaam, Meck Sadiki, alitembelea katika kikosi cha Stara na
kuwapa moyo wa kuhakikisha kuwa wanafanya vyema mbele ya Ivory Coast na kufufua
matumaini ya kufuzu katika michuano hiyo.
Alitumia
nafasi hiyo pia kuwapa salamu za Rais Jakaya Mrisho Kikwete, juu ya kuwafunga
Ivory Coast, ambaye ndio anayeongoza kundi C, ambaye pia imewasili Tanzania
ikiwa na lengo la kushinda katika uwanja wa ugenini.
“Tunataka
ushindi na sio kuogopa majina ya wachezaji hawa wa Ivory Coast maana ni wenye
miguu kama nyie, huku tukiamini kuwa Stars mnaweza kufanya vyema na kulitangaza
Taifa katika mpira wa miguu, hivyo fanyeni bidii,” alisema Sadik.
Nahodha
wa Stars, Juma Kaseja, aliwahakikishia Watanzania kuwa watacheza kufa na kupona
katika kuhakikisha kuwa wanafanya vyema katika mchezo huo muhimu kwao.
“Tunatambua
moyo wa uzalendo uliopo kwa Watanzania dhidi yetu, hivyo nitashirikiana na
wenzangu katika kuona tunashinda katika mechi ya Ivory Coast katika uwanja wetu
wa nyumbani.
“Tunajiamini
kwa kiasi kikubwa kuwa tunaweza kufanya vizuri katika mchezo wetu huu, hivyo
tunaomba Watanzania waje kwa wingi kushangalia kwa ajili ya kuwafunga Ivory
Coast,” alisema Kaseja.
Stars
inanolewa na kocha wake Kim Poulsen, huku akiwa na shauku ya kuona timu yake
inafuzu katika michuano ya Kombe la Dunia, endapo itashinda katika mechi zake
zilizosalia.
No comments:
Post a Comment