https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, June 09, 2013

Viongozi wa CCM waaswa kukipigania chama chao ili kiendelee kushika dola Tanzania


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
VIONGOZI wa matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameaswa kufanya kazi zao kwa umakini na uangalifu katika kuhakikisha kuwa chama chao kinaendelea kupendwa na Watanzania.
 Calist Lyimo akizungumza katika semina hiyojana
 Semina ya CCM jana ilikuwa poa
Wana CCM Makumbusho wakiwa kwenye semina jana.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Uenezi wa CCM, wilaya Kinondoni, Mwinyimkuu Sangalaza, katika semina iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Kata ya Makumbusho, ambapo pia ilifunguliwa na MNEC wa CCM Kinondoni, Calist Lyimo.

Akizungumza na viongozi wa matawi hayo katika  semina hiyo, Sangalaza, alisema kuna haja ya viongozi wa matawi hayo, ambao ndio mhimili wa chama kufanya kazi kwa umakini na kukipigania zaidi na zaidi katika harakati za kisiasa nchini.

Alisema Tanzania kwa sasa inakabiriwa na changamoto nyingi za kiuongozi, hasa kwa kuona baadhi yao wanafanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wenye pesa na kuendeleza fitina.

“Sisi tupo ndani ya CCM, lakini hatuna mchango wowote maana wengi wao tunapenda chuki na kuweka visasi dhidi ya wenzetu, hivyo ufanisi unakuwa mdogo katika kazi zetu.

“Naomba tuache hayo kwa ajili ya maslahi ya CCM katika kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na ule Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015,” alisema.

Katika semina hiyo, watoa mada walikuwa ni Holestes Damino, Muhidin Said, Ibrahim Hella na Sangalaza, mara baada ya kufunguliwa na MNEC, Lyimo, wakati walioandaa ni Kata ya Makumbusho kwa kupitia viongozi wao Hashim Athuman, Fatuma Sadiki, Abdi Abbasi Haidery Suwea, chini ya uratibu wa Mchumi wa Kata ya Makumbusho, Yusuph Shaban Mhandeni kwa maslahi ya CCM.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...