Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENKI ya CRDB leo imezindua
huduma ya ‘Fahari Huduma’ ya kuweka na kutuma pesa kwa njia ya wakala, badala
ya kwenye matawi ya benki kama ilivyozoeleka.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki
ya CRDB, DK. Charles Kimei, akizungumzia huduma mpya ya kibenki ya Rafiki
Huduma mbele ya wageni waalikwa leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa THT wakicheza katika uzinduzi huo leo asubuhi.
Akizungumza katika Uzinduzi
huo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei, alisema kuwa kwa huduma
hiyo, wateja wao watapata huduma karibu na wanapohitaji.
Alisema kuwa wakala wote
watakaosajiliwa na benki yao,
wataweza kutuma pesa, kuweka au kulipa bili zao kwa njia ya urahisi zaidi,
ikiwa ni ubinifu mzuri kwa ajili ya wateja wao.
Uhondo wa THT ukiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki
ya CRDB, DK. Charles Kimei, akizungumzia huduma mpya ya kibenki ya Rafiki
Huduma mbele ya wageni waalikwa leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
“Ni watu wachache wanaopata
fursa za kibenki, ila kwa sasa kila mtu anaweza kuhudumiwa mahala popote, maana
wateja wataweza kupata huduma za kibenki kwa mawakala.
“Sisi CRDB tunaamini kuwa
tutaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wateja wetu, ndio maana wakati wote
tunakaa na kuwaza njia ya kuwahudumia kwa ufanisi wateja wetu,” alisema Kimei.
Katika uzinduzi huo, wasanii
kutoka nyumba ya kulea na kukuza vipaji ya Tanzania House of Talents (THT)
walifanya shoo kwa wageni waalikwa katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.
No comments:
Post a Comment