https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, June 04, 2013

Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge ' ajifua kwa pambano lake dhidi ya Bahati Mafyela

Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge akiwa katika pozisheni
Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge akifanya mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake
Kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito wakati wa mazoezi yaliyofanyika kigogo mburahati Dar es Salaam Bonge anajiandaa na mpambano wake na Bahati Mafyela.
Kocha Kwame Mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge jinsi ya kutupa makonde mfululizo wakati wa mazoezi yake.

Kocha Kwame Mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito.

Na Mwandishi Wetu
Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mafyela, mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Idi pili jijini Dar es salaam katika ukumbi wa friends Corner Manzese

akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji Waziri Rosta amesema mpambano huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hawo wanatafutana kwa mda mrefu sana na sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo

Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu  wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini

aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini

Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa akuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo naisi mambo yatakuwa safi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...