Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa asili nchini, Saida Kalori, amezushiwa kifo, huku
mwenyewe akilizungumzia hilo kwa kusema kuwa wanaotaka afe wataanza wao kwanza.
Saida Karoli, pichani
Taarifa hizo zilianza kuzagaa usiku wa juzi na kuzua hofu kwa wadau wa
muziki Tanzania, ukizingatia kuwa tayari kumekuwa na mfululizo wa vifo vya
wasanii, akiwapo Albert Mangweha ‘Ngwair, Langa Kileo na wengineo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mbeya Vijijini, mwimbaji huyo wa
Mapenzi Kizungu zungu, Chambua Kama Karanga na nyinginezo, alisema kuwa
habari za kifo chake ni za uzushi na zimelenga kuwachanganya wapenzi wake Tanzania na duniani kwa ujumla.
habari za kifo chake ni za uzushi na zimelenga kuwachanganya wapenzi wake Tanzania na duniani kwa ujumla.
Alisema kuwa sio kweli kama amekufa kama habari hizo zilivyotolewa, hivyo
wanaotaka afe wataanza wao kwanza kabla yake.
“Sio kweli kuwa nimekufa, hivyo wadau waelewe kuwa nipo salama, huku
Mbeya vijijini,” alisema Saida na kuzipinga kwa nguvu zote habari hizo
zinazosema kuwa amefariki kwa ajali ya boti na wengine kudai kuwa amepata ajali
ya gari.
Saida anaheshimika kwa nyimbo zake nyingi zilizomuweka katika kilele cha
mafanikio ya muziki hapa nchini, akiimba zaidi nyimbo za asili ya Bukoba na
kujizolea mashabiki lukuki.
No comments:
Post a Comment