Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe mwenye miwani akiwasili Polisi jana.
Freeman Mbowe wa pili kutoka kulia, akijadiliana jambo baada
ya kujisalimisha Polisi.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
HALI ya mvutano kati ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), pamoja na Jeshi la Polisi, unaendelea kushika kasi huku mwenyekiti
wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwa mkali kama mbogo na kusema kuwa hawezi
kuwasilisha ushahidi wa mlipuko wa bomu kwa polisi isipokuwa kwa Tume Maalum ya kimahakama.
Madai ya Mbowe yamepokelewa kwa hisia tofauti, huku wale
wasiounga mkono harakati za wapinzani wakichukulia kama njia ya kulisumbua
jeshi la Polisi pamoja na kutafuta umaarufu mbele ya jamii.
Jana Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alitangaza hali ya hatari kwa
wananchi watakaokaidi agizo halali la jeshi la Polisi, jambo litakalosababisha
polisi watumie nguvu, ikiwapo kuwatandika virungu.
"Wapigwe tu, maana ndio njia halali ya kutuliza vurugu, hivyo
nashauri wananchi wasiwe wakaidi maagizo halali ya Polisi," alisema Pinda
na kuzua maswali kwa wananchi hasa waliokuwa upande wa Chadema.
No comments:
Post a Comment