Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Shinyanga Emporium (1978),
leo imezindua Bajaj mpya aina ya Piaggio ambayo haitumii mafuta mengi, hivyo
kuwa mkombozi kwa wananchi wote, wakiwamo wafanyabiashara wa Bajaj.
Nishit
Peter, Meneja wa Tawi lililopo karibu na Mlimani City, akitoa maelekezo
kwa wateja wake waliotembelea kwenye uzinduzi wa bajaj aina ya Piaggio, leo jijini Dar
es Salaam.
Nishit Peter, Meneja wa Tawi lililopo karibu na Mlimani City, akitoa maelekezo kwa mteja wake katika uzinduzi wa bajaj aina ya Piaggio, leo jijini Dar es Salaam.
Tukio la uzinduzi wa bajaj hiyo
lilifanyika leo mchana katika tawi lao lililopo karibu na Mlimani City,
likihudhuliwa na watu mbalimbali, wakiwamo wafanyabiashara wa bajaj jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Meneja wa Biashara wa Kampuni hiyo, Ritesh Monani, alisema kuwa bajaj
hiyo ni mkombozi kwa watu wote, hasa matumizi yake mazuri ya mafuta, ikitumia lita moja kwa kilomita 32, huku tenki lake likiwa na uwezo wa kubeba lita 10.
Alisema bajaj hiyo kwa sasa
inapatikana kwa Shilingi Milioni 5.7, ambapo mteja atafurahia mpangilio mzima
wa uundwaji wake, sambamba na upatikanaji wa vipuri vyake Tanzania.
“Tumekuwa tukipokea maoni ya
wateja wetu Tanzania, hivyo bajaj hii ni nzuri kwa watu wote, jambo linalotupa
imani kuwa itapokelewa kwa mikono mizuri sambamba na usalama wake,”alisema.
Usafiri wa bajaj hutumiwa sana
duniani, hasa nchini India, huku kwa jijini Dar es Salaam, ukijulikana kama
moja ya usafiri unaomuwezesha mtu kufika haraka anapokwenda.
No comments:
Post a Comment