Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya
vijana ya Coastal Union inatarajia kuelekea jijini Arusha, Julai nne mwaka huu
tayari kuanza kwa michuano ya Kombe la Rolling Stone, iliyopangwa kuanza
kutimua vumbi Julai sita.
Kikosi cha vijana wa Coastal Union kikijifua uwanjani.
Coastal
wanakwenda Arusha huku wakiwa na kumbukumbu ya kushika nafasi ya pili katika
mashindano yaliyofanyika mwaka jana nchini Burundi na kuitangaza vyema
Tanzania.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka Tanga, Meneja wa timu hiyo ya vijana, Abdulrahaman
Ubinde, alisema kuwa wapo tayari kwa mapambano katika mashindano hayo.
Alisema
watafika jijini Arusha siku mbili kabla ya kuanza kwa mashindano ya Rolling
Stone, huku wakiwa na shauku ya kufanya vyema na kuonyesha cheche zao katika
mpira wa miguu.
“Tumepanga
kuelekea Arusha Julai nne kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ambayo mwaka
jana tulishika nafasi ya pili na kushangaza wadau wengi wa soka.
“Tupo
imara na hakika vijana watafanya kazi nzuri katika mashindano hayo yanayoleta
mwamko wa aina yake, ukizingatia kuwa Coastal Union imejiweka katika soka la
ushindani,” alisema.
Katika
patashika ya Ligi ya Tanzania Bara iliyomalizika mwezi uliopita, Coastal Union
ambao imepandisha wachezaji sita wa vijana, ilimaliza ikiwa katika nafasi ya
sita, huku ubingwa ukinyakuliwa na Yanga.
No comments:
Post a Comment