Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Ahmed Kipozi
ameitaka jamii kuakikisha inashughulikia suala la kuwalinda watoto ikiwemo
suala la ukatili, mila kandamizi na utumikishaji usiofaa.
Mkuu wa Wilaya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, akizungumza jambo juu ya haki za watoto wilayani humo leo.
Watoto wakicheza mchezo wa kufukuza kuku.
Kipozi alisema hayo jana jumapili alipokuwa mgeni rasmi
wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika inayofanyika kila mwaka Juni
16.
Akihutubia wananchi, pamoja na watoto wakiwemo kutoka
shule mbalimbali za msingi za Wilaya hiyo, alisema kuwa Jamii inajukumu kubwa
ya kuakikisha sula la ulinzi linatekelezwa kwa pamoja hasa katika kumlinda
mtoto.
“Kumlinda mtoto na mila kandamizi ni jukumu letu, nasi
hatuna budi kuwaakikishia hilo pamoja na kutokeza vitendo viovu dhidi yao”
alisema Kipozi.
Pia alieleza kuwa wajibu wa kila mmoja ni kuakikisha watoto
wanakuwa kwenye ustawi bora katika makuzi yao ilikuweza kutimiza malengo yao
mbalimbali pindi watakapofika ukubwani.
kwa upande wake, mmoja wa wazee wa Mila wilayani hapa,
Rashid Yusufu Sekamba alisema kuwa watahakikisha wanaachana na mila
potofu ilikuendana na wakati ikiwemo suala la unyago kwa watoto wa kike.
“Tumesikia sana kilio chenu watoto, juu ya mila potofu hasa
unyago, tutachukua hatua na hata kulimaliza.
.Mimi sijui huko kwenye unyago wanafundisha mambo gani, ila
kama unamcheza mtoto bado yupo shule, ni lazima aende akajaribu kwa vitendo
hili si sawa. Sasa unadhani hili ni sawa?, si sawa wazee wa mila tutaangalia
namna ya kuachana nalo,” alisema Sekamba.
Katika maadhimisho hayo, ambayo yaliratibiwa na
Halimashahuri ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, Mkuu wa Wilaya
alikabidhi baiskeli moja ya walemavu (wheelchair), pamoja na kupokea kandambili
pea 300, vyote vilivyoolewa na Asasi ya TRACED.
Sherehe za mwaka huu za mtoto wa afrika yenye kauli mbiu,
“Kuondoa mila potofu zenye kuleta madhara kwa watoto: Ni jukumu letu sote”.
Kwa upande wao wajumbe mbalimbali waliotoka asasi za kiraia
ndani ya wilaya hiyo walipongeza shughuli hiyo.
Asasi hizo ni pamoja na HELP Foundation, Mkombozi, TRACED,
HakiMtoto Foundation, BAKA, Compassion na wengine wengi.
Kwa upande wa watoto hao waliweza kuelezea na kutoa kero
mbalimbali dhidi ya vitendo wanavyofanyiwa na jamii ikiwemo unyanyasaji na
ukatili huku wakiomba kutambua watoto ni taifa la leo hivyo linahitaji
kulindwa.
Kupitia risala yao, watoto hao mbele ya DC, walitaka
kuthaminiwa na kuwekewa ulinzi, kusikilizwa na yale yote yanayohusu haki ya mtoto.
No comments:
Post a Comment