https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, June 09, 2013

Madee asema hajawahi kuona Mangwair akigombana


Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Morogoro
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, Ahmad Ally Madee, amesema kuwa hajawahi kuona ugomvi mzito kati ya marehemu Albert Mangweha Ngwair na msanii mwingine Tanzania.
Madee akiingia Uwanja wa Jamhuri kumuaga marehemu Ngwair, aliyozikwa Alhamisi mkoani Morogoro.

Madee aliyasema hayo mkoani Morogoro katika mazishi ya Ngwair, yaliyofanyika katika Makaburi ya Kihonda Kanisani na kuhudhuriwa na watu wengi, yakitanguliwa na shughuli ya kuaga Uwanja wa Jamhuri.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Madee alisema kuwa hajawahi kuona ugumvi mzito wa Ngwair na wasanii wengine, hivyo inaonyesha namna gani maarehemu aliishi kwa upendo.

Alisema katika sanaa kumekuwa na migogoro ya hapa pale, lakini kama Ngwair aliweza kugombana na watu, basi ilikuwa kimya kimya, kama alivyowahi kuimba enzi za uhai wake.

“Simsifii Ngwair kwasababu leo ametangulia mbele ya haki, ila kwakweli Tanzania tumepoteza msanii nyota na aliyekuwa  na uwezo wa aina yake, huku kila mmoja akimpenda na kumheshimu sana.

“Zaidi ni jinsi alivyoweza kuishi kwa upendo na wasanii wote, ukizingatia kuwa sisi kwenye fani hii wakati mwingine unalumbana na mtu, lakini kwa Ngwair yeye hilo suala sijawahi kulisikia,” alisema Madee.

Madee anayetesa na wimbo wa Pombe Yangu, pia ni Rais wa kundi la Tip ‘Connection’ lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, akijulikana pia kwa jina la Rais wa Manzese.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...