Na Jumaa Mussa, Muheza
MWENYEKITI wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameijia juu serikali kwa
madai kuwa inajiendesha kwa hasara, sambamba na kutumia Trilioni 2.8 za
makusanyo ya kodi za ndani za wananchi kwa ajili ya Shirika la Umeme Tanzania
TANESCO.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe
Mbowe aliyasema hayo
wilayani Muheza, mkoani Tanga jana, alipokuwa katika safari za kichama akifunga
kampeni za uchaguzi wa udiwani zilizofanyika katika Kata ya Genge Wilayani
Muheza Mkoani Tanga.
Alisema fedha hizo
zinatumika katika kuendeshea mitambo ya shirika hilo kuwalipa makampuni
yanayozalisha umeme pamoja na kununua mafuta mazito kwa ajili ya kueneshea
mitambo ya kuzalishia nishati hiyo hapa nchini.
Mbowe alisema kwa siku
moja pekee Shirika hilo hutumia sh Bil 5.4 kwa ajili ya kununua mafuta mazito
ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme ambao umeme huo unazalishwa na
makampuni binafsi, huku akisema fedha hizo zinatumika vibaya bila kuwa na akili
za kuliongoza Taifa lenye changamoto za kila aina.
"Hii sio seerikali na
inapenda kujiendesha kwa hasara kila siku ya Mungu, maana kumekuwapo na mianya
ya utafunaji wa fedha za umma bila sababu za msingi, hivyo lazima wananchi
tujuwe kuwa huu ni mwisho wao na hatuwezi tena kuwa wajinga,” alisema Mbowe.
“Nashangazwa na
serikali hii isiyosikivu tunatumia kodi za wananchi katika kulipa makampuni
yatuzalishie umeme wakati vipo vyanzo vya uhakika vya maji ambavyo vinagharama
nafuu vinaachwa.
“Wananchi wa Muheza
mnakazi moja tuu ya kukiondoa chama cha Mapinduzi CCM madarakani ili muweze
kuunganisha nguvu za maendeleo zuinazofanywa na CHADEMA katika mikoa mingine
nchi kwa sasa,” alisema Mbowe.
Mgombea wa udiwani kwa
tiketi ya Chadema ni Josepha Komba, huku akiwataka watu watakubali mabadiliko
ya uongozi katika kata hiyo kwa kumpa nafasi ya kushinda katika Uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment