Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga, amewataka makocha
kuhakikisha wanaibua vipaji vya watoto ili kuwa na vipaji vingi baadaye.
Mhitimu wa kozi ya ukocha wa mpira wa miguu kwa ngazi ya
pili, Moses Mkandawile akipongezwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini,
Leodgar Tenga kwenye sherehe zilizofanyika jana Uwanja wa Taifa.Kulia ni
Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo na (kushoto) Mkurungenzi wa Ufundi TFF,
Sunday Kayuni.
Tenga alikuwa mgeni
rasmi katika ufungaji wa kozi hiyo ya ngazi ya pili iliyofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo
iliyoendeshwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Dar es Salaam (DRFA), ilianza
Juni 3 huku ikishirikisha zaidi ya makocha 58.
Tenga alisema Bara la
Afrika ndilo bara lenye upungufu mkubwa wa wachezaji watoto, tofauti na mabara
mengine, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya soka.
“Hili ndilo bara
ambalo lipo nyuma katika kuibua vipaji, mfano nchi ya Ujerumani pekee ina
watoto zaidi ya milioni moja ambao wanaandaliwa, lakini hapa sijui kama
wanafika hata idadi hiyo, hivyo kuna changamoto kubwa katika hilo,” alisema.
Aliwataka kuhakikisha
wanayatumia mafunzo hayo katika kuleta mabadiliko katika soka hapa nchini,
ambapo pia aliwapongeza kwa kushiriki katika kozi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa
DRFA, Almas Kassongo amesema kozi hiyo itakuwa mkombozi wa makocha kusaidia
timu zao kufanya vizuri na kuendeleza mchezo huo nchini.
"Napenda kutoa
shukrani zangu za dhati kwa Rais wa TFF kwa kukubali kuwa nasi licha ya
majukumu mengi aliyonayo, lakini niseme tu kwamba kozi hii imekuwa ya mafanikio
kutokana na kushirikisha wachezaji wengi wa zamani," alisema.
Baadhi ya washiriki
waliohitimu kozi hiyo ni pamoja na Moses Mkandawile, Shedrack Nsajigwa, Ibrahim
Masoud Maestro, Shaffih Dauda, Rahel Pallangyo, Ally Yusuph Tigana, Emanuel
Gabriel, Jemedari Said, Benard Mwalala, Edibily Lunyamila, Seleman Matola na
wengineo.
No comments:
Post a Comment