https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, June 07, 2013

Mamia wamzika mume wa Khadija Kopa ambaye pia ni diwani mjini Bagamoyo, wakiwapo wasanii, viongozi wa chama na serikali



Na Kambi Mbwana, Bagamoyo
MUME wa mwimbaji wa muziki wa taarabu hapa nchini, Khaidija Kopa, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magomeni, Jafari Ally, ameszikwa jana katika makaburi yaliyopo mjini Bagamoyo.

 ''Pole mwaya''. Ndivyo anavyoonekana kusema Karima Chichi Mhandeni wa tatu kutoka kulia, akimfariji Khadija Kopa, katika msiba wa mume wake aliyezikwa leo Bagamoyo.
 Waombolezaji wakiwa katika msiba wa mume wa Khadija Kopa, leo mjini Bagamoyo.
Jeneza la Jafary Ally likiswaliwa mbele ya nyumba yake mjini Bagamoyo leo. Wa nne kutoka kulia ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwan Kikwete, akiungana na waislamu wenzake kuuswalia mwili wa Diwani wa Kata ya Magomeni, mjini Bagamoyo.
 Safari ya kuelekea makaburini ikaanza. Aliyebeba mwenye fulana ya mistari ni Yusuphed Mhandeni, Mchumi wa Kata ya Makumbusho CCM, jijini Dar es Salaam.

Mazishi yake yalidhuhuriwa na watu wengi, wakiwamo viongozi wa vyama vya siuasa, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Serikali pamoja na wasanii wengi waliokwenda kumpa pole Kopa.

 Khadija Kopa aliyefunikwa akifarijiwa kwa msiba wa mume wake mjini Bagamoyo.
 Mwili wa marehemu Jafary Ally ukiingizwa kaburini leo saa tisa alasiri mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Mchumi wa Kata ya Makumbusho (CCM), Yusuph Shaban Mhandeni, Yusuphed Mhandeni mwenye fulana ya mistari akibeba jeneza la Jafary Ally, mume wa Khadija Kopa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magomeni, Bagamoyo, katika mazishi yake yaliyofanyika leo mjini Bagamoyo.

Msiba wa Ally ulitikisa katika viunga vya mji wa Morogoro, huku miongoni mwa viongozi wa juu waliohudhuria akiwa ni Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa.

Akizungumza kwa machungu makubwa, Khadija Kopa, alisema amejisikia uchungu mume wake kufariki huku akiwa nje ya jiji la Dar es Salaam, huku akirejea akimkuta mumewe ni marehemu.

Alisema kuwa msiba wa mumewe umempa uchungu mkubwa, huku akiamini kuwa utaendelea kuwa kichwani mwake kwasababu ya kuondokewa na mume wake aliyempenda.

“Nimeuamia sana na msiba huu wa mume wangu,” alisema Khadija Kopa, huku akibubujikwa na machozi.

Aidha, Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Bagamoyo, Shukuru Mbato, alitumia muda mwingi kuwata Watanzania wakiwamo wakazi wa Bagamoyo kuishi kwa upendo sambamba na kumuombea marahemu aishi kwa amani katika maisha yake mapya.

“Sisi tulimpenda sana, ila Mungu ndio muweza wa yote, hivyo sisi kama binadamu lazima tukubali matokeo,” alisema Mbato.

Watu kutoka sehemu mbalimbali, wakiwamo wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza kwa wingi katika mazishi ya Ally, ambaye pia ni mume wa Khadija Kopa.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...