https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, May 08, 2013

Siri za Utajiri wa Kichawi wa Kabila la Wakinga mkoani Iringa zafichukaHAYA ni maoni na mtazamo wa mchambuzi wa masuala ya Uchumi na Biashara Albert Nyaluke Sanga aliyotoa katika mahojiano yake na wataalamu wa chuo Tumaini walipomtembelea nyumbani kwake Iringa kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali ya kimaisha.
Albert Nyaluke Sanga, mchambuzi wa biashara na uchumi Tanzania

Mwezi uliopita kuna wataalamu wa masuala ya biashara kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini walifika ninapoishi kunihoji kwa dodoso la kiutafiti; lengo likiwa ni kujua.

Je, ni kwa nini watu wa kabila la Wakinga wanafanikiwa sana kibiashara?" Waliuliza maswali mengi lakini swali lao kubwa lilikuwa ni hili:
"Unaongeleaje dhana inayoaminika ya kwamba wakinga wengi wanafanikiwa kibiashara kwa sababu ya ushirikina?

Majibu yangu kwao kwa swali hili yalikuwa kama hivi: "Ushirikina upo na unaweza kumfanikisha mtu kibiashara. Hata hivyo ushirikina upo katika makabila yote Tanzania. Cha kujiuliza hapa ni hiki:

Kwa nini wakinga wengi wanaonekana kutumia mwanya huu wa ushirikina kufanikisha biashara zao?' 'Ikiwa kila kabila kuna ushirikina ni kwa nini makabila mengine yasiutumie ushirikina wao kutajirika kama inavyosemwa kwa wakinga?'

Bila shaka kuna "KITU CHA ZIADA" kinachowafanya wakinga wafurukute hata kuamua kutumia mwanya wa ushirikina maadamu wafanikiwe tofauti na makabila mengine; ambayo licha ya kuushikilia ushirikina lakini hawautumii kibiashara.

Hii ina maana hata UKIONDOA USHIRIKINA wanaotuhumiwa nao wakinga; bado wakinga wana nafasi kubwa kufanikiwa kibiashara kwa sababu ya kile

KITU CHA ZIADA cha kufurukuta, kupambana na kutorudi nyuma. Niliwaeleza kwa kirefu historia ya imani za waganga wa Ukingani walivyoanza kutoa huo utajiri; nikawaeleza mabadiliko ya vizazi vitatu vya wakinga na namna ilivyoleta mapinduzi kiimani na kibiashara. Baada ya hayo nilihitimisha kwa kuwaeleza hivi:

"Ukiacha issue ya ushirikina, kuna siri zinazofanya wakinga wafanikiwe sana kibiashara baadhi yake ni hizi, 1) hawatumii zaidi ya wanachoingiza, 2) wanaheshimu akiba kiasi kwamba MKINGA yupo tayari kufa na njaa lakini asiguse akiba (inaitwa ekhefumbato),3) wana nidhamu kubwa mno ya matumizi ndio maana wengi wamebatizwa jina la "mabahiri" (kupewa hela ya bure bure ama kuhongwa na mkinga itakubidi ufanye kazi ya ziada sana!!!)

4 Hawa jamaa wanapokuwa kwenye stage ya utafutaji huwa wanajitenga kabisa na starehe ndio maana wengi hudhaniwa kuwa ni "washamba" 5) wanasaidiana sana kwa kupeana mitaji na 6 hawana WIVU KABISA mkinga mwenzao anapoinuka kibiashara.

Albert Sanga ni mchambuzi wa masuala ya biashara na Uchumi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...